The House of Favourite Newspapers

Jahazi Msagasumu Waacha Historia Dar Live Jana

KUNDI la Muziki wa Taarab lisilo na mpinzani Bongo, Jahazi Modern sambamba na Mfalme wa Singeli, Msaga Sumu jana waliandika historia ya aina yake baada ya kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye shoo ya Sikukuu ya Idd el Hajj ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

9

Msanii wa Jahazi akifanya yake kwenye shoo hiyo iliyotawaliwa na burudani za kufa mtu

Katika shoo hiyo ambayo ilianza kufunguliwa na wasanii chipukizi wanaofanya vizuri kwenye gemu la muziki wa Bongo Fleva wakiwemo Lamuzika Vijana Classic, AD Classic, Tamaduni, Topito na MC wa Dar Live, Brighton Darada, Jahazi walipafomu ngoma zao zote kali zikiwemo Nipe Stara na Nilijua Nitasema.

Kwa upande wa mfalme wa muziki wa uswahilini, Msaga Sumu yeye pia alikamua ngoma zake zote kali bila kusahau Unanitega Shemeji, Mama wa Kambo na Chura.

1 Mwanamuziki kutoka Jahazi, Reila Rashindi akikamua katika shoo hiyo.

2Mfalme wa Muziki wa Singeli Bongo, Msaga Sumu akiwarusha mashabiki wa Singeli jana

3Msaga Sumu akifanya yake jukwaani

4Umati wa mashabiki waliohudhulia kwenye shoo hiyo wakizidi kuburudika

  1. Msanii chipukizi wa nyimbo za asili, Topito akionyesha uwezo wa kucheza kwenye shoo hiyo

5Msanii chipukizi wa nyimbo za asili, Topito akionyesha uwezo kwenye shoo hiyo

6Topito akizidi kuwapagawisha mashabiki

Mpiga picha: Issa Mnally/Boniphace Ngumije.

Comments are closed.