The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Awapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanayoifanya kuwaletea watanzania maendeleo

0

 

Waziri Mkuu Mkuu wa Jamhuri wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa.

Waziri Mkuu Mkuu wa Jamhuri wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na hadhara ya wafanyakazi walikusanyika kushiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani mkoani Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, tarehe 01, Mei, 2024.

Majaliwa amesema kuwa, siku ya Wafanyakazi Duniani Mei Mosi ni siku maalum kwa ajili ya wafanyakazi kutafakari na kutathmini namna walivyotekeleza majukumu yao, kwa kuzingatia malengo waliyojiwekea katika mwaka husika.

Amesema kuwa siku hiyo inatoa fursa kwa wafanyakazi wote duniani kuweka mipango kwa ajili ya mwaka unaofuata na ndiyo maana inafanyika kipindi ambacho nchini nyingi duniani zinakuwa katika maandalizi ya Bajeti.

Amesema hayo leo Jumatano Mei Mosi, 2024)wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani inayofanyika kitaifa mkoani Arusha, kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid. Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo ni Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“siku hii ni muhimu sana na inatukumbusha wajibu wetu wafanyakazi wa kujadiliana kwa pamoja changamoto zilizopo katika utendaji wetu wa kazi na kuzitafutia ufumbuzi kwa pamoja na hatimaye kuleta tija katika maeneo ya kazi”.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewapongeza watumishi wote kwa kazi kubwa wanayoifanya katika kuwaletea watanzania maendeleo. “Sisi sote ni mashahidi wa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka mitatu kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia na kijamii”

Kaulimbiu ya maadhimisho hayo ni “Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na Kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha”

”RAIS SAMIA AMESEMA ATASEMA JAMBO KUHUSU KUONGEZA MSHAHARA” – MAKAMU MPANGO MBELE ya WAFANYAKAZI


 

Leave A Reply