JAHAZI, TMK KUTOANA JASHO PASAKA DAR LIVE

Yah TMK Modern,

KUNDI la Muziki wa Taarab, Yah TMK Modern, Aprili Mosi (Sikukuu ya Pasaka) linatarajiwa kutoana jasho na kundi kongwe la muziki huo,Jahazi Modern katika shoo bab’kubwa ya Usiku wa Mwisho wa Ubishi itakayofanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

 

Yah TMK Akizungumza na Mikito Nusunusu, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba alisema, kundi la Yah TMK lililo chini ya Mkubwa Fella litaongoza mashambulizi yake jukwaani huku mkali wao Omary Tego akiwadatisha wapenzi wote wa muziki watakaojitokeza.

 

“Wale wapenzi wote wa Muziki wa Pwani, Muziki wa Mwambao Pasaka hii si ya kukosa, Dar Live pekee itahakikisha kila kitu kinaenda sawa na niwaambie tu, nyimbo kibao zitatawala jukwaani kutoka Yah TMK ikiwemo ya Figisufi gisu,Siwaguni Wala Siwakohoi, Sina Pupa pamoja na Hashuo la Mke Mwenza,” alisema KP.

 

Jahazi Modern

 

 

Jahazi Modern KP aliongeza pia, Jahazi Modern watakuwepo kutoa burudani ya kihistoria ambapo wakiwa chini ya Prince Amigo watahakikisha kila shabiki anayeingia anapata burudani ya aina yake.“Vipo vibao vingi vitakavyorindima katika usiku wa wabishi kutoka Jahazi,chini ya Amigo mashabiki watarajie kusikia vibao kama

 

Tiba ya Mapenzi pamoja na Acheni Porojo. Pia watapata kuzisikia nyimbo zote zilizotamba na zinazoendelea kutamba kama vile Mpenzi Chocolate.

 

”Man Fongo Mbali na uwepo wa makundi hayo ya Taarab, kutakuwa pia na shoo ya kibabe kutoka kwa wakali wa Singeli, Man Fongo, SholoMwamba na Dulla Makabila. “Mara tu ya Jahazi na Yah TMK kushuka jukwaani, tutakuwa na Man Fongo ambapo siku hiyo atawaonesha Singeli inaimbwaje na inachezwaje huku akizindua ngoma yake mpya ambayo ataitaja kwa hiyo fanya ufike tu usikie ngoma zake zote kali kuanzia Hainaga Ushemeji, Nani Asiyependa hadi Safi Tu.

 

”Sholo Mwamba, Makabila “Singeli itakuwa imeteka ukumbi mzima, Dar yote itahamia Dar Live kwa saa kadhaa. Sholo Mwamba na Dulla Makabila watahakikisha kila shabiki anacheza na kuimba nao pamoja nyimbo zao zote,” alimaliza KP.

 

Mtonyo sasa Fanya uwahi mapema usije kujilaumu geti likifungwa! Kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa kiduchu sana buku saba yaani shilingi 7,000 hukumichezo mbalimbali ya watoto ikiwemo kuogelea itafanyika kuanzia saa nne asubuhi hadi 12 jioni kwa mtonyo wa buku tatu yaani shilingi 3,000.

Mikito Nusunusu


Loading...

Toa comment