The House of Favourite Newspapers

Jaji Mahakama Kuu Rugazia Afariki Dunia

JAJI Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania,  Projestus Aloyce Rugazia (pichani),  amefariki dunia Agosti 04, 2019 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Msiba upo nyumbani kwake Kinondoni- Dar es Salaam na ratiba ya taratibu za kuaga na mazishi itajulikana Kesho, Agosti 05, 2019. Marehemu alizaliwa Agosti 28, 1954 mkoani Kagera, alianza kazi rasmi Januari 01, 1983, akiwa Hakimu Mkazi.
Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Machi 28, 2003 na alistaafu Agosti 28, 2016 akitokea Mahakama Kuu-Divisheni ya Ardhi.
 Mahakama ya Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA,  JINA LAKE LIHIMIDIWE
IMETOLEWA NA :
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,
MAHAKAMA YA TANZANIA.

Comments are closed.