The House of Favourite Newspapers

Jamaa Raia wa Marekani Atupwa Jela Miaka Minne kwa Kumpiga Teke Afisa wa Polisi

0
Robert Gilman akiwa Gerezani

MAHAKAMA moja katika mji wa magharibi mwa Russia ya Voronezh, Jumanne imemuhukumu raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 28 kifungo cha miaka minne na miezi sita jela, kwa kumpiga teke Afisa wa Usalama.

 

Kamati inayofanya uchunguzi kuhusu matukio makubwa ya uhalifu imesema katika taarifa, “Mwanaume huyu ambaye alipinga hatua za kisheria zilizochukuliwa na mamlaka, alitumia vurugu dhidi ya Afisa wa Polisi aliyekuwa zamu na kumpiga mateke mara kadhaa.”

 

Mmarekani huyo aliyetajwa na Shirika la Habari la Serikali ya Russia kama Robert Gilman, anakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, wakili wake amesema.

 

Wakili Valery Ivannikov, ameongeza kuwa mteja wake anapanga kuwasiliana na maafisa wa Marekani ili kupanga ubadilishanaji wa wafungwa.

Leave A Reply