The House of Favourite Newspapers

Jamaa Yamkuta Baada ya Kukojoa Hapa

0

JESHI la Polisi mjini Kakamega wamemkamta jamaa mmoja kwa kumpiga na kumjeruhi mwenzake aliyepuuza onyo kwa umma kutokojoa hadharani.

 

Katika kisa hicho, Jared Otieno,30, alikasirishwa baada ya mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 24, kupuuza onyo la “Kojoa Hapa Uone!” lililokuwa limeandikwa kwenye ukuta.

 

Katika taarifa kwenye Twitter, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai ( DCI) nchini humo imesema kuwa mwathiriwa hakuwa amemaliza kujisaidia wakati Otieno alitokea na kumpiga mangumi na mateke.

 

Mateke na mangumi ya Otieno yalimn’oa meno ya mwathiriwa na kuwacha uso wake ukiwa umevimba. Wasamalia wema walijaribu kumtuliza Otieno aliyekuwa lakini walisindwa.

 

Mwathiriwa ambaye alijeruhiwa vibaya, alishindwa hata kufungua mdomo wake sababu ya majeraha makubwa na kukimbizwa katika Hospitali Kuu ya Kakamega kwa matibabu.

Leave A Reply