The House of Favourite Newspapers

Jamani Kaka Cheni …Ndiyo Nini Sasa?!-14

1

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Eti akaniambia atarudi msala huo ukipoa. Nilijaribu kulalamika nikimsihi asifanye hivyo lakini alikataa. Akasogea hadi mlangoni kwa kunyata, kisha akaufungua mlango na kutoka kwa tahadhari. Mara nikasikia mlango wa nyumba kubwa nao ukifunguliwa.

JIACHIE MWENYEWE…

 

 

Nilishtuka sana, nikatoka kitandani na kwenda hadi mlangoni nikijua kaka Cheni anadakwa na baba au mama.

Niliufunga mlango wangu polepole sana ili aliyetoka asijue kama mlango ulikuwa wazi…

“We Cheni unatoka wapi muda huu?” ilikuwa sauti ya mama ikimuuliza kaka Cheni…

“Kutembea mama.”

“Kutembea?! Hivi wewe unataka uwe unaambiwa kwa njia gani lakini? Si jana tu baba yako ametoka kukwambia hataki kukuona ukitembea usiku!”

“Nilikwenda kumtazama rafiki yangu mmoja anaumwa mama.”

“Nani?”

“Mtoto wa mzee Abdallah Mzee.”

“Wewe unamtafuta baba yako,” nilimsikia mama akisema huku akitembea kuja usawa wangu. Mlango wangu uligongwa…

“Ngo ngo ngo!”

“Nani wewe?” nilijifanya kuuliza kwa sauti ya kutoka uzungizini huku nikipiga mwayo…

“Ulikuwa unafungua mlango ulitaka kutoka?” alisema mama. Niliguna kwanza…

“Mh!”

Kisha nikamjibu…

“Hapana mama.”

“Mbona mlango wako ulikuwa unalia kitasa?”

“Mh!” niliguna tena mwenyewe.

Nikajiuliza…

“Ina maana mama alisikia kitasa cha mlango wakati nafunga funguo…

“Kweli mama ni kiboko,” nilisema moyoni.

“Mama sijataka kutoka,” nilisisitiza huku nikiwa najikunja ili nilale vizuri.

Mama aliingia ndani kwake, akafunga mlango.

Sasa nikawa najiuliza, nimcheki kama Cheni kwenye simu au? Maana aliniachia njiani. Lakini moyoni nikawa nasema sitakuwa na amani kwani ilionekana kama mama au baba mmoja wao alikuwa na machale na ndiyo maana mama alitoka.

Machale yenyewe ni kumfuatilia kaka Cheni kama anatoka  kwenda kutembea au la!

Nikiwa nawaza, meseji kwenye simu yangu ikaingia, nikaifuata simu kwenye stuli ili sasa hata nikisoma meseji hiyo, nilale na simu yangu kitandani…

“Oya sasa?” ilitoka kwa kaka Cheni…

“Mh! Soo!” nilimjibu.

“Soo la nini bwana? hawezi kutoka tena.”

“Wee! Akitoka je?”

“Najua hawezi. Kama una wasiwasi we njoo kwangu,” aliniambia kaka Cheni jambo ambalo sikukubaliana nalo hata kwa asilimia kumi na moja…

“Kwako siji kaka Cheni,” nilimjibu.

“Utakuja tu,” alijibu hivyo mpaka nikakasirika sasa. Kwa nini kaka Cheni ananilazimisha hivi.

“Siji,” nilimjibu tena huku mwisho nikiweka alama kibao za kushagaa kama hizi!!!

Kulipita ukimya, lakini na mimi hali yangu ilibadilika sana, nikawa najihisi mpweke kuwa peke yangu mle chumbani hasa nikichukulia kwamba, kaka Cheni aliniachia njia ya panda baada ya kukurupushwa na mdingi.

Niliwaza sana, ilifika mahali nikawaza hata ningekuwa kwangu ningekuwa huru zaidi kwani hata dhambi ya mimi na kaka Cheni isingekuwepo lakini ndiyo hivyo tena! Kama kaka Cheni ambaye ni mtoto wa kiume bado alikuwa akiishi nyumbani, sembuse mimi binti?! Hata ningekuwa na pesa nisingekubaliwa.

Jamaa yangu naye, nilishamwambia alete barua ya posa nyumbani ili tuwe huru lakini amekuwa akinizungusha tu, kesho…kesho…mara, wiki ijayo..wiki ijayo…

Basi, ikawa kila dakika nashika simu yangu kuiangalia nikiamini kaka Cheni amenitumia meseji lakini wapi! Ilibidi mimi ndiyo nimuulize yeye…

“Umelala?”

Meseji hiyo haikujibiwa, nikaamua kupiga…

“Eee!” alipokea…

“Umeshapitiwa na usingizi?”

“Ningepitiwa na usingizi ningepokea simu?”

“Bwana! Mi nakuuliza…”

“Sijalala…unasemaje?”

“Kwani hujui?”

“Sijui…we si umesema huwezi kuja huku kwangu!”

“Sasa baby unadhani mi nikija huko halafu baba akitoka itakuaje? Afadhali uje wewe maana mimi wana staa wa kuingia kwangu,” nilimwambia kaka Cheni kwa sauti ya chini sana…

“Kwa hiyo nije?”

“Njoo. Lakini hulali?”

“Itategemea.”

“Hapana baby…tuelewane kabisa, ukija usilale. Unajua ukilala ni hatari zaidi.”

“Haya silali.”

“Poa, karibu baby nimekumisi sana mwenzio, yaani we acha tu sweet.”

Nilikata simu, nikaenda mlangoni na kuufungua mlango kisha nikarudi kitandani kumsubiria.

Mwili wote ulikuwa na joto lenye baridi. Kama nilihitaji shuka lakini pia kama nilihitaji mwili wa mwanaume wenye joto kali. Nikajikuta najikunyata peke yangu.

Mlango ulifunguliwa polepole nikajua sasa kaka Cheni anawawasili  si nikajiachia kwa raha zangu! Ili kudeka kwa kaka niliama kugeukia ukutani ili akifika yeye ndiyo aniamshe kwa staili yoyote atakayoitaka, hata kunibusu au vyovyote vile.

“Wewe umefungua mlango ili uende wapi au nani aingie muda huu?”

 

Je, nani aliyeuliza hivyo? Na nini kiliendelea? Usikose kusoma wiki ijayo.

1 Comment
  1. Peter says

    Majanga!

Leave A Reply