The House of Favourite Newspapers

Jamii Sports Club yaadhimisha Nyerere day kwa kuchangia damu

0

2.Wanajoggingi walioshiriki uchangiaji damu huo wakiwa katika picha ya pamoja.

Wanajogging  walioshiriki uchangiaji damu huo wakiwa katika picha ya pamoja.

3.Wanajongi wakiwa katika picha ya furaha.

Nyuso za furaha na hamasa tupu

4.Dazeti la Championi likisomwa na wanajogging.

Gazeti la Championi likisomwa na wanajogging.

5.Mmoja wa maktari kutoka Hospitali ya Parestina akitoa ushauri nasaha kwa mmoja wa washiriki wa zoezi la uchangiaji damu.

Mmoja wa madaktari kutoka Hospitali ya Palestina akitoa ushauri nasaha kabla ya kutoa damu. 

6.Zoezi la uchangiaji damu kutoka kwa Madaktari wa Hospitali ya Parestina na Mwananyamara wakitoa huduma kwa wachangiaji damu salama.

Madaktari wa Hospitali ya Palestina na Mwananyamala wakitoa huduma kwa wachangiaji damu salama.

7.Utoaji damu ukiendelea.

Utoaji damu ukiendelea.

8.Daktari wa utoaji damu akimuandaa mwanajogging kwa ajili ya kutoa damu.

Daktari wa utoaji damu akimuandaa mwanajogging kwa ajili ya kutoa damu.

NA DENIS MTIMA/GPL

JAMII Sports Club yenye maskani yake Sinza jijini Dar, kwa kushirikiana na vilabu mbalimbali vya michezo vya jijini Dar, vimeungana na kuratibu bonanza la pamoja ikiwa ni njia ya kuadhimisha miaka 16 tangu kifo cha aliyekuwa Baba wa Taifa, Hayati Julius Kambarage Nyerere, ambapo pamoja na mambo mengine, vimeendesha zoezi la kuchangia damu.

Akizungumza na mwandishi wetu, wakati wa shughuli hiyo, mratibu wa mfuko wa uchangiaji damu uliofanyika kwenye kiwanja cha Shule ya Msingi Mashujaa jijini Dar, Henry Katabazi, amesema lengo la kujumuika na kuandaa bonanza hilo, ni kujenga uhusiano mwema, kujenga afya na kukumbuka mchango wa Mwalimu Nyerere kama mwasisi wa taifa letu.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Manispaa ya kinondoni,  Dk. Aziz Msuya,  akizungumza na washiriki wa mabonanza hayo, amewapongeza kwa namna walivyoweza kujitolea katika uchangiaji damu salama na kusaidia wenye uhitaji huo na kwamba waendelee na moyo huo.

Baadhi ya vilabu vingine vya michezo vilivyoshiriki zoezi hilo ni pamoja na Mbagala Jogging , Mburahati Jogging , Tandale Jogging  Ubungo Jogging Club  na Msasani Jogging Club.

Leave A Reply