January Makamba Atoa Kauli ya Kwanza Twitter

Aliyekuwa Waziri ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi wakiwa wanatabasamu.

Baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba na nafasi yake kumteua mwingine, Makamba ametoa kauli yake ya kwanza baada ya uamuzi huo.

 

Taarifa ya Ikulu iliyotoka leo Jumapili na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Julai 21, 2019 imeeleza Rais Magufuli amemteua George Simbachawene kuchukua nafsi ya Makamba aliyedumu katika nafasi hiyo tangu Desemba mwaka 2015.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Makamba ameeleza kupokea taarifa hiyo na kuahidi kutoa kauli yake siku zijazo “Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa.

Nitasema zaidi siku zijazo,” ameandika Makamba ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) huku akiambatanisha na picha yake akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi wakiwa wanatabasamu


Loading...

Toa comment