The House of Favourite Newspapers

JENEZA, KABURI WATAKAMOZIKWA MARIA NA CONSOLATA – PICHAZ

ZOEZI la uchimbaji wa kaburi kwa ajili ya maziko ya mapacha walioungana, marehemu Maria na Consolata limefanyika katika Makaburi ya Masista wa Shirika la Bikira Maria wa Consolata Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa leo Jumanne, Juni 5, 2018.

Wananchi walio wengi wamejitokeza kuandaa nyumba ya milele ya mapacha hao walioaga dunia usiku wa Jumamosi iliyopita katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakitibiwa.

Aidha, mafundi katika Kampuni ya Mandela wamefanya maandalizi ya mwisho ya utengenezaji wa jeneza litakalotumika kuwazikia mapacha haao.

Shughuli ya kuandaa jeneza hilo imefanyika katika eneo la Sido Manispaa ya Iringa, kama picha zinavyoonyesha.

Mazishi ya mapacha hao yanatarajjwa kufanyika kesho Jumatano kwenye makaburi ya Masista Tosamaganga mkoani Iringa.

 

PICHA NA HILALI DAUDI | GLOBAL TV ONLINE, IRINGA

 

 

Comments are closed.