The House of Favourite Newspapers

JENGO LA KAMPUNI LAGEUZWA DANGURO

KANGI Lugola (Waziri wa Mambo ya Ndani) upo? Ndivyo walivyohoji wakazi wa Sinza-Mori jijini Dar karibu kabisa na Kituo cha Mafuta cha Big Bon wakionesha kuchoshwa na vitendo vinavyofanya ndani ya nyumba yenye geti linalojinasibu kuwa ni kampuni (jina tunalihifadhi kwa sasa), lakini ndani inafanyika biashara ya ngono.

TUJIUNGE NA WATOA TAARIFA

Awali, Gazeti la Ijumaa Wikienda kupitia Kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) lilielezwa kuwa, nyumba hiyo imekuwa tatizo la muda mrefu kwani wanawake hao wanaofanya biashara ya ngono, hufanya hadharani pindi tu giza linapoanza kuingia, muda ambao watoto wanakuwa hawajalala.

“Yaani hili ni tatizo, wanafanya vitendo vya hovyo sana, wanajipanga nje ya geti hilo ikifika tu saa moja usiku muda ambao watoto wetu wanaosoma mbali ndiyo wanakuwa wanarejea majumbani.

“Sasa hebu fikiria, wanavaa nguo za nusu utupu, wanajipanga nje ya geti hilo, watoto wetu watajifunza nini? Huyu Waziri Lugola ambaye tumeona moto wake kwa nini asije kushughulikia suala hili?” Alihoji mmoja wa watoa taarifa.

Mtoa taarifa huyo alizidi kutiririka kuwa, mbali na kuvaa nguo za nusu utupu, eneo hilo ni kero kwa watu wanaozunguka maana matendo kama ya uvutaji sigara, unywaji wa pombe unasababisha usumbufu kwa familia zilizopo jirani na nyumba hiyo.

“Lakini sasa, hao wanaojipanga pale nje, baadhi wana vyumba ndani ya jengo hilo na ukiongea naye vizuri unakwenda kumalizana naye humo, wapo wengi, tena mabinti wabichii,” alidai mtoa habari huyo.

OFM MZIGONI

Kama ilivyo desturi ya OFM, mara baada ya kupewa taarifa hizo, kitengo hicho kiliketi na kupanga mikakati maalum ya kwenda kufanya uchunguzi.

Katika hatua za awali, siku ya kwanza, OFM ilijiridhisha pasi na shaka kweli nyumba hiyo ina geti lenye jina la kampuni huku pia kukiwa na ujumbe unaokataza watu kusimama nje ya geti hilo, lakini hata hivyo, warembo hao wanaofanya biashara ya ngono giza linapoingia, husimama bila wasiwasi wowote wakiwa nusu utupu.

Siku hiyo pia OFM waliweza kubaini kuwa kuna vigogo mbalimbali ambao wanaingia na kutoka katika nyumba hiyo kwa kupitia mlango wa uani ambao upo jirani na baa.

SIKU YA PILI

Mara baada ya kuwaona warembo hao, siku ya pili makamanda wa OFM walifika eneo hilo muda wa saa mbili asubuhi na kujaribu kuingia ili kuona kama kweli biashara ya ngono inafanyika, lakini muda huo ilidaiwa kuwa wengi wanakuwa wamelala na wateja wao.

“Unajua hawa huwa wanakula vichwa short time (muda mfupi), lakini ikifika muda wa saa kumi usiku huwa wanachukua vichwa vya kulala, sasa ukija saa mbili asubuhi kama hii, wanakuwa bado wamelala na wateja wao,” alidai mmoja wa wahudumu wa baa iliyo jirani na nyumba hiyo bila kujua anazungumza na kamanda wa OFM.

Humo ndani, OFM ilishuhudia vyumba kibao visivyopungua 20 ambavyo vimejipanga kwenye jengo la kushoto na pia ndani humohumo kuna jengo lingine lililopo upande wa kulia.

SIKU YA TATU

Huku ikiongeza ‘mitambo maalum’ ya unasaji wa picha za mnato na mjongeo (video), OFM ilizingira nyumba hiyo kuanzia ndani hadi nje na kunasa matendo machafu yanayotendeka ndani humo.

Mmoja wa OFM aliyetolewa chambo cha kuthibitisha biashara ya ngono eneo hilo alikwenda na kujifanya anahitaji huduma ambapo alishuhudia vyumba vingi, baadhi ya warembo wakiwa wamesimama mlangoni na kujishebedua kibiashara huku vingine vikiwa vimefungwa.

Mazungumzo ya OFM huyo na mmoja warembo hao wanaojiuza yalikuwa hivi;

OFM: Shilingi ngapi fastafasta?

Mrembo: Raundi moja elfu 20, ukitaka ya pili n’takufanyia elfu hamsini.

OFM: Mimi nina shilingi elfu kumi tu nataka raundi mbili huwezi kunipunguzia?

Mrembo: Acha ubahili, we kaka vipi?

Baada ya OFM kutishia kama anakwenda chumba cha pili ambacho kilikuwa na mrembo mwingine mlangoni, mrembo huyo alikubali kwa shingo upande hela hiyo.

Ili kujiridhisha, OFM ilimlipa dada huyo na kuingia ndani kukagua mazingira yaliyopo ambapo ndani ya chumba hicho kuna viatu vingi, nguo, mapochi na mazagamazanga mengine, hali inayoashiria mrembo huyo anaishi humo kwa muda mrefu.

Baada ya mrembo huyo kuanza kufungua vifungo vya shati la kamanda wa OFM na kutaka kuanza kutoa huduma, kamanda huyo alijifanya amepokea simu na kutoka zake eneo hilo.

MWENYE JENGO ANAFAHAMU UCHAFU HUU?

Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumsaka mmliki mwenye jengo hilo ili kutaka kujua kama anayo taarifa juu ya kutumika kama danguro lakini halikufanikiwa kumpata mhusika. Jitihada zinaendelea.

Hata hivyo, makachero wa OFM waliwahi kuzungumza na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nzasa, Jacob Nyamaka ambaye alisema kimsingi analifahamu tatizo la eneo hilo korofi, lakini kila anapolishughulikia kwa kuwafukuza madadapoa hao wamekuwa wakirudi tena hivyo kuomba msaada serikalini ngazi ya wilaya (Kinondoni) imsaidie.

OFM ILIWAHI KUPASHUGHULIKIA

Awali, jengo hilo getini lilikuwa limeandikwa jina la gesti na ikaelezwa kuwa, biashara ya ngono ilikuwa ikifanyika ndani ambapo OFM waliwahi kutinga wakiwa na Polisi na kuwanasa mabinti kibao ambao walitiwa mbaroni.

Siku nyingine, mmoja wa makamanda wa kike wa OFM akiwa kwenye uchunguzi wa biashara hiyo eneo hilo, machangu hao walimshtukia ambapo walimteka na kumpeleka ndani ya moja ya chumba cha jengo hilo na kutaka kumfanyia umafia kabla ya Polisi kuvamia na kumuokoa.

HATUA ZICHUKULIWE!

Kwa muda mrefu eneo hilo limekuwa korofi, ukiuliza soko maarufu la ukahaba jijini Dar, eneo hilo lililopo Mori karibu na kituo cha mafuta ni hatari hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni chini ya ACP Jumanne Muliro lichukue hatua stahili haraka kabla mambo hayajaharibika.

STORI:Waandishi Wetu, DAR

Comments are closed.