The House of Favourite Newspapers

Jenner, Ronaldo, Beyoncé Waongoza kwa Mkwanja Instagram

Tokeo la picha la Kylie Jenner
Kylie Jenner

STAA wa televisheni na mwanamitindo wa Marekani, ameongoza orodha ya mastaa wenye mkwanja mkali katika mtandao wa Instagram (Instagram Rich List) ambapo posti yake moja ina thamani ya Dola milioni moja.

Picha inayohusiana

Kardashian

Wanaofuatia ni  Kim Kardashian (Dola 720,000), Kendall Jenner (500,000) na Khloe Kardashian (480,000).

Katika soka ni Cristiano Ronaldo (750,000),  Neymar (600,000), Lionel Messi (500,000), katika muziki ni  Selena GomezBeyoncé na Justin Bieber walioshika nafasi za pili, tano na saba kwa mikwanja ya 800,000, 700,000 na 630,000 kwa kufuatana.

Dwayne “The Rock” Johnson yuko nafasi ya sita akiwa mwigizaji pekee katika kumi bora kwa mkwanja wa 650,000.

Comments are closed.