The House of Favourite Newspapers

Jerry Silaa Ajisalimisha, Atolewa Nje – Video

0

BAADA ya wito wa kukamatwa Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa uliotolewa jana, hatimaye leo Ijumaa, Agosti 27, 2021 Mbunge huyo amefika akiwa peke yake na kuingia ukumbi wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge akiwasubiri wajumbe wa Kamati hiyo ili kuendelea na shauri lake.

Silaa amefika katika Ukumbi huo majira ya saa 1 asubuhi akiwa peke yake bila kusindikizwa na polisi huku akiwa na begi dogo mkononi na chupa ya maji ya kunywa na kuelekea moja kwa moja kwenye Jengo la Utawala. Ilipofika majira ya saa 4 akaingia kwenye Ukumbi wa Kamati ya Maadili kabla ya Mwenyekiti na wajumbe wake kuingia.

Alipoingia mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Emanuel Mwakasaka akaamuru mbunge huyo atoke nje ya Ukumbi na Asubiri kuitwa kama utaratibu unavyosema.

Leave A Reply