The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Mapinduzi Guinea Laagiza Benki Zote Kufunga Akaunti za Serikali

0

Mamlaka ya kijeshi ya Guinea, imeamuru benki kufungia akaunti zote zinazohusiana na serikali ili “kupata mali za serikali”.

 

Jeshi ambalo lilishika udhibiti wa nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, linasema agizo hilo linaathiri akaunti za taasisi na watu binafsi wa serikali inayomaliza muda wake. Maofisa wa juu wa serikali ya Rais aliyeondolewa madarakani Alpha Condé hawataweza kutumia akaunti zao.

 

Viongozi hao wa mapinduzi walichukua madaraka Jumapili, na wamesema wanataka kumaliza ufisadi uliokithiri, ukiukwaji wa haki za binadamu na usimamizi mbaya.

 

Jumuiya ya kiuchumi ya eneo la Magharibi mwa Afrika ECOWAS ambayo inataka katiba kufuatwa imetuma ujumbe wa kutaka kufanya mazungumzo na mamlaka ya Guinea. Jumuiya hiyo imetaka Rais Condé ambaye ameshikiliwa na jeshi kuachiwa huru.

Leave A Reply