The House of Favourite Newspapers

Jeshi la Polisi Laungwa Mkono Dhidi ya Ajali za Barabarani

0

 

Mashindano ya kimataifa ya “VIA CREATIVE” yanayolenga kuelimisha wanafunzi wa shule za msingi kujifunza kuhusu usalama barabarani yazinduliwa rasmi na kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania kupitia Total Energies Foundation kwa kushirikiana na Nafasi Art Space jijini Dar es Salaam katika tukio lililofanyika shule ya msingi ya Buza. Mafunzo hayo yataanza Oktoba 9 – 20 huku fainali ya kitaifa kufanyika tarehe 13 Oktoba na Kimataifa tarehe 13 Novemba.

Kampeni hii inawapa mwanya wanafunzi wa shule za msingi kuelezea mawazo yao kwa kutumia ujumbe wa kujikinga kwa wale wawazungukao kwa njia ya michoro ya mabango na kuelimisha vijana kuhusu usalama wa barabarani kupitia njia ya sanaa ambapo washindi watapokea zawadi kuanzia 100,000Tsh hadi 200,000Tsh.

Mwisho wa mashindano, kikundi kitakachoshinda kitashiriki katika fainali za kimataifa
pamoja na washindi wengine kutoka nchi mbalimbali katika fainali itakayofanyika Paris, Ufaransa.

Mkurugenzi Mkuu wa TotalEnergies nchini Tanzania, Mamadou Ngom alinukuliwa, ‘tumedhamiria kukuza uelewa wa matumizi za alama za barabarani kuanzia ngazi ya chini ili kulea jamii inayojali matumizi sahihi ya barabara, hivyo basi ni matumaini yetu hii itakuwa chachu ya kuisadia na jamii nzima inayotuzunguka dhidi ya ajali za barabarani’.

Nae mgeni rasmi, Mrakibu Msaidizi wa jeshi la polisi Asulwisye Edward Mwakyonike ambaye pia ni Mkuu wa usalama barabarani wa wilaya ya kipolisi ya Mbagala, alisema, ‘tunaishukuru sana kampuni ya TotalEnergies kupitia foundation yake kulisaidia jeshi la polisi kupanua wigo wa elimu ya usalama barabarani, ni matumaini yetu shindano hili litadumisha mshikamano miongoni mwa jamii dhidi ya ajali zinazoweza kuepukika’.

Kwa mwaka huu wanafunzi kutoka shule 35 za jijini Dar es salaam na 20 za Bagamoyo watakutana katika shindano la kuchora lenye lengo la kuelimisha kuhusu usalama wa barabarani. Katika kipindi hiki cha mafunzo, wanafunzi wakifanya kazi kwenye makundi ya watu 5 na kutengeneza mabango kuhamasisha vijana, wanafunzi wenzao na watu wazima kubadili tabia zao na msimamo wao ili kuongeza uwajibikaji katika swala zima la usalama wa barabarani kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu.

Kila shule watachaguliwa wanafunzi 10 ambao watakuwa mabalozi wa usalama barabarani na kushiriki mashindano ya kitaifa ya uchoraji mabango yenye ujumbe wa kujikinga na ajali za barabarani.

Leave A Reply