The House of Favourite Newspapers

MSEMAJI ZIMAMOTO AFANYA ZIARA GLOBAL GROUP

Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja (wa pili kulia) akimsikiliza kwa makini mmoja wa wafanyakazi wa  Global Group (aliyevaa shati la bluu) kitengo cha usambazaji  wakati wa ziara yake ya kukuza mahusiano alipotembelea kampuni hiyo mapema leo.
Ofisa Habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Sajenti  Nasibu Mgoso, akisaini kitabu cha wageni wakati walipofika ofisini hapo.
Mhariri wa Gazeti la Amani wa Kampuni ya Global Group, Erick Evarist (katikati), akitoa ufafanuzi kwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Inspekta, Joseph Mwasabeja, (wa pili kulia), jinsi Kampuni ya Global Group inavyoendesha shughuli zake kupitia vyombo mbalimbali vilivyopo chini ya kampuni hiyo wakati wa ziara yake ya kukuza mahusiano mapema leo.
Mhariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist (kulia) akiwatembeza katika ofisi hiyo kwenye vitengo mbalimbali vya Globabl Group.
Erick Evarist akiwaonyesha bango lenye magazeti yanayozalishwa na kampuni hiyo.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja (kushoto) akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa, Amran  Kaima.
...Akisalimiana na mwandishi wa habari wa Magazeti Pendwa, Boniphace Ngumije(kulia)
Mhariri wa Gazeti la Amani, Erick Evarist(wa pili kushoto) akiutambulisha ugeni huo kwa wahariri wa magazeti ya michezo ya Championi.
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Usanifu kurasa, Bahati Haule (kulia).
Msemaji Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja, (kulia) akisalimiana na Meneja Mkuu wa  Global Publishers, Abdallah Mrisho (kushoto) alipotembelea kampuni hiyo.

 

 

MSEMAJI wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja akiambatana na ofisa habari wa jeshi hilo, Sajenti Nasibu Mgoso, leo wametembelea Kampuni ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar kuona utendaji kazi wa kampuni hiyo ambayo huchapisha magazeti pendwa pamoja na ya michezo.

 

Akiwa kwenye ofisi hizo, Inspekta Mwasabeja aliweza kutembelea idara mbalimbali za magazeti Pendwa ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi na kubadilishana mawazo mawili matatu na wahariri pamoja na waandishi wa magazeti hayo.

 

Kama hiyo haitoshi, Inspekta Mwasabeja alitembelea pia idara ya usambazaji, idara ya wasanifu kurasa, Gazeti la Spoti Xtra, Gazeti la Championi, Global TV Online pamoja na kitengo cha Tehama (IT).

Pia, aliweza kuzungumza na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho kisha kufanya uchambuzi wa habari na Global TV Online utakaoruka hapo baadaye, saa 12 na nusu jioni.

 

Comments are closed.