MSEMAJI ZIMAMOTO AFANYA ZIARA GLOBAL GROUP
MSEMAJI wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Inspekta Joseph Mwasabeja akiambatana na ofisa habari wa jeshi hilo, Sajenti Nasibu Mgoso, leo wametembelea Kampuni ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar kuona utendaji kazi wa kampuni hiyo ambayo huchapisha magazeti pendwa pamoja na ya michezo.
Akiwa kwenye ofisi hizo, Inspekta Mwasabeja aliweza kutembelea idara mbalimbali za magazeti Pendwa ambayo ni Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Risasi Jumamosi na kubadilishana mawazo mawili matatu na wahariri pamoja na waandishi wa magazeti hayo.
Kama hiyo haitoshi, Inspekta Mwasabeja alitembelea pia idara ya usambazaji, idara ya wasanifu kurasa, Gazeti la Spoti Xtra, Gazeti la Championi, Global TV Online pamoja na kitengo cha Tehama (IT).
Pia, aliweza kuzungumza na Meneja Mkuu wa Global, Abdallah Mrisho kisha kufanya uchambuzi wa habari na Global TV Online utakaoruka hapo baadaye, saa 12 na nusu jioni.
Comments are closed.