The House of Favourite Newspapers

Jeshi Laahidi Kurejesha Hali ya Usalama

0


LUTENI Kanali Paul-Henri Damiba aliyeongoza mapinduzi yaliyomtoa Madarakani Rais Roch Kabore ametoa hotuba yake ya kwanza kwa taifa hilo na kusema jeshi litakutana na makundi mbalimbali ya Jamii kujadili mchakato wa kufanya mageuzi.

 

Amesema Burkina Faso inahitaji msaada wa washirika wa kimataifa kuvuka hali ya sasa, pia ameahidi suala la usalama litapewa kipaumbele na Jeshi.

 

Wanachama wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wanakutana leo Januari 28, kujadili mapinduzi ya Burkina Faso.

 

Burkina Faso ni nchi ya tatu ya Afrika Magharibi mapinduzi ya  kijeshi katika miaka ya hivi karibuni. Guinea na Mali zimewekewa vikwazo na jumuiya ya kikanda ya Ecowas ili kuzishinikiza kurejea kwa utaratibu wa kikatiba.

Leave A Reply