| Manchester, England
KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola kwa sasa ana furaha kutokana na mwenendo wa timu yake kwenye Ligi Kuu England.
City haikuwa na matokeo mazuri kwa kipindi kirefu msimu huu na hali imekuwa mbaya sana wakati ambapo mshambuliaji wa timu hiyo, Sergio Kun Aguero, anakosekana uwanjani.
Lakini sasa anaonekana kuwa na imani kuwa timu hiyo inaweza kufanya vizuri bila kuwa na mchezaji huyo baada ya kumsajili mshambuliaji raia wa Brazil, Gabriel Jesus.
Wikiendi iliyopita, City waliingia uwanjani na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, dhidi ya Swansea kwenye mchezo wa ligi kuu uliokuwa mkali na wa kuvutia.
Kwa mara ya kwanza, kocha wa City alimweka kwenye benchi Aguero na kumuanzisha Jesus ambaye hakika hakumuangusha kwani alionyesha kiwango cha juu sana na kuifungia timu hiyo bao safi katika dakika za mwisho na kuwapa ushindi huo ambao umewapeleka hadi nafasi ya tatu kwenye ligi.
Kabla ya bao hilo, Jesus pia ndiye aliyefunga bao la kwanza la timu yake na kuendelea kuonyesha kuwa yeye ni staa kwenye timu hiyo na Ligi Kuu England kwa ujumla.
Awali wakati anajiunga na timu hiyo hakupewa nafasi kubwa lakini kwa muda mchache tu ameshaonyesha kuwa yeye ni mchezaji mahiri kwenye ulimwengu huu wa soka.
Wachambuzi wengi wa soka wa England wamekuwa wakimfananisha kijana huyo na enzi za mshambuliaji hatari wa zamani wa England, Michael Owen kutokana na kasi yake na uwezo wa juu wa kupachika mabao.
Kiwango cha mchezaji huyo kimeanza kuonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Aguero akaondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu.
Jesus kwa sasa ameshapachika mabao matatu kwenye michezo minne ambayo ameichezea timu hiyo akitokea Palmeiras ya Brazil.
City walimsajili mchezaji huyo kwa kitita cha pauni milioni 27, ambapo aliwasili kwenye timu hiyo akionekana kuwa hawezi kuwa mchezaji hatari.
“Kwangu nafikiri anaweza kufanya vizuri zaidi ya hali ilivyo kwa sasa, kutumika chini ya michezo 10 kwenye Ligi K u u England bado hakuwezi kukufanya wewe ukaonekana kuwa mchezaji mahiri.
“Nimpongeze kwa kiwango anachoonyesha kwa sasa na naamini kuwa anaweza kutusaidia kufanya vizuri zaidi kwenye michezo mingine ijayo.
“Tulipomsajili tuliamini kuwa ni mchezaji mahiri na hili limeanza kuonekana kwenye michezo michache tu ambayo ameichezea timu hii, naamini atakuwa bora zaidi msimu ujao,” alisema kocha wa City, Pep Guardiola.
Kinda huyu mwenye umri wa miaka 19, amekuwa akitajwa kuwa anaweza kuwa staa ajaye kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil ambayo kwa sasa imekuwa ikisuasua.
Jesus ambaye alijiunga na timu hiyo kwenye usajili wa Januari, alikuwa ameshafanya mambo makubwa kwenye Ligi Kuu ya Brazil.
Hadi sasa bado siyo mchezaji mahiri sana kwa upande wa rekodi akiwa amefanikiwa kucheza michezo 83 kwenye klabu yake ya zamani ya Palmeras na michezo minne akiwa na City.
Takwimu zinaonyesha kuwa anaweza kuwa mchezaji hatari sana siku za usoni kutokana na wastani mzuri wa kupachika mabao kwani hadi sasa ameshafunga mabao 31 kwenye mchezo hiyo.
Imekuwa ikiaminika kuwa anaweza kuwa staa wa timu ya Taifa ya Brazil muda mchache u j a o a k i w a a m e s h a i chezea michezo sita na kufunga mabao manne.
Kumbukumbu kubwa aliyonayo kwenye soka ni kutwaa medali ya dhahabu mwaka 2016 akiwa na Brazil.
Comments are closed.