The House of Favourite Newspapers

Jezi Mpya za Manchester United Yavuja katika Tamasha la Glastonbury

0
Rapper Harrison James Armstrong almaarufu ‘Aitch’ wa Manchester, England

Wakati Manchester United wakitarajia kuzindua jezi zake kwa ajili ya msimu ujao wiki ijayo siku ya Jumanne lakini tayari jezi hizo zimevuja baada ya Rapper Harrison James Armstrong almaarufu ‘Aitch’ wa Manchester, England kuonekana akiwa amevaa jezi hiyo wakati akitumbuiza katika tamasha la Glastonbury hivi karibuni.

Aitch ambaye ni shabiki wa Mashetani hao wekundu toka utotoni, aliwapa mashabiki hakikisho kamili la jezi hiyo wakati wa tamasha hilo la muziki huku akiwa ameiandika jina ‘Big Shell’ ikiwa na namba 40 mgongoni mwake.

Jezi hiyo, iliyotawaliwa na rangi nyekundu ya kawaida, ina muundo unaovutia wa maua ya Lancashire yaliyotapakaa kote sehemu ya mbele ya jezi.

Pia kwenye kola na mikononi imepambwa na mistari ya rangi nyeusi maarufu ya Adidas ambayo iko kwenye nafasi yake ya kawaida.

Leave A Reply