The House of Favourite Newspapers

JIDE YAMKUTA YA GIGY MONEY

DAR ES SALAAM: BAADA ya kutupia picha zake tata mtandaoni, mkongwe wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Jide’ yamemkuta majanga yaliyowahi kumkuta msanii Gift Stanford ‘Gigy Money’ ya kuchongewa kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Jide alikutwa na kisanga hicho hivi karibuni mara baada ya kutupia picha yake kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram inayomuonesha akiwa amevaa gauni jeusi lililoacha wazi sehemu kubwa ya maumbile yake nyeti.

Gauni hilo lilikuwa limeacha sehemu kubwa ya paja la kushoto likiwa wazi kuanzia sehemu ya kisigino hadi kiunoni.

 

Kama hiyo haitoshi, gauni hilo liliacha kitovu chake nje jambo ambalo liliwashtua mashabiki wengi ambao wamemzoea Jide akiwa kwenye mavazi ya heshima hasa kutokana na umri wake kuwa mkubwa (miaka 39).

Kufuatia kitendo hicho, maoni mbalimbali yaliyotupiwa kwenye ukurasa huo yalimuandama Jide kwa kuonesha amefanya jambo ambalo halifanani na ukongwe wake katika sanaa pamoja na umri wake.

“Dada yangu hapo umebugi sana maana wewe ni kati ya wasanii wanaoangaliwa sana hasa kwa kujiheshimu kwako lakini katika hili sister umebugi,” alichangia jamaa anayejiita Benardmakabita.

Mbali na mchangiaji huyo, wachangiaji wengi walionekana kumpa maneno makali Jide wakidai hakupaswa kufanya hivyo kwani hata kama ni ‘kiki’ ya wimbo au tukio lolote anataka kulifanya, hapaswi kujidhalilisha kwani yeye jina lake ni kubwa.

“Huku ni kujivunjia heshima aliyojiwekea kwa miaka zaidi ya kumi sasa kwenye gemu ya Bongo Fleva, kwa kweli Jide tunayemjua si huyu. Basata mko wapi? Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) hamlioni hili? Tunaomba mumshughulikie huyu maana ataharibu wasanii wengi wanaochipukia,” alichangia mchangiaji mwingine aliyejiita Kindoki.

 

Wachangiaji waliofuata baada ya Kindoki, wengi waliamua kuchachamaa na ishu ya Basata na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) wamshughulikie kama walivyomchongea Gigy Money ambaye alipewa onyo na Basata lakini hata hivyo aliendelea kujiachia kihasara katika matamasha yake.

Komenti hizo za kumchongea zilimchoma Jide ambaye aliamua kuwajibu kwa kuwawekea picha yake nyingine mpya akiwa na msanii wa Bongo Fleva, Sunday Mangu ‘Linex’ na kuweka ujumbe wa kuwajibu wale waliomkosoa katika suala zima la maadili.

“Hivi wale watu wa maadili mbona picha za hivi huwa hamlike wala ku-comment kwa wingi mkiwekewa? Haya maadili hayo hapo sasa, inakuwaje? Mbona hamsifii? Ila binadamu ni wanafiki sana sijapata kuona,” aliandika Jide katika ukurasa wake.

Juzi, Amani lilimvutia waya Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza ili kuweza kumsikia ana maoni gani kuhusu picha hiyo ya Jide lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Stori: Mwandishi Wetu, Amani.

EXCLUSIVE: NIKKI Kuhusu PAULA Kufeli “Ni Ujinga Tu”

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.