The House of Favourite Newspapers

JIFUNZE KUWEKA ULINZI KWENYE FLASH YAKO

Kama wewe ni mzoefu sana wa kutumia flash na memory kadi utakuwa umeshakutana  na tatizo la ‘write protectio’(ulinzi) ambalo haliruhusu chochote kuingia kwenye Flash wala kutoka(nikimaanisha ku copy wala kutuma chochote)

 

Leo hii utajifunza jinsi ya kuiwekea flash/memory kadi yako’write protectio’(ulinzi) na kuiondoa.(Tatizo la flash kama picha hapo chini)

 

 

ANGALIZO:Hakikisha unao uwezo wa kutumia kompyuta kwa ufasaha kwasababu ukikosea kuna uwezekano ukaua Flashi/memory kadi yako.

 

FWATA HATUA HAPA(JINSI YA KUWEKA – KUTOA)

 

 

1:Chomeka Flash/Memory Card kwenye Kompyuta

 

 

2:Bonyeza Batana ya Window na R (picha hapo juu)

 

 

3:Baada ya kubonyeza utaona picha kama hiyo hapo juu

 

 

4:Andika ‘CMD’ kwenye kibox kama inavyoonekana kwenye picha halafu bonyeza Ok

 

 

5:Baada ya kubonyeza itatokea kitu kama picha hapo juu

 

 

6:Andika ‘diskpart’kwa herufi ndogo halafu bonyeza Enter

 

 

7:Zitatokea Window mbili kama inavyoonekana kwenye picha juu.

 

 

8:Pale kwenye DISKPART andika ‘list disk’ (zitatokea disk zako zote hapo)

 

 

9:Chagua Disk yako kati ya zinazoonekana kwa kuandika chini ‘select disk 1 au 2.halafu bonyeza Enter(hakikisha unajua ukubwa wa flash/memory yako)

 

 

10:Hapo chini andika hivi, ‘attributes disk set readonly’ halafu bonyeza Enter (itaonekana kama picha hapo juu na maneno yanayosomeka chini yake, ‘Disk Attributes set Successfully’.

 

Mpaka hapo utakuwa tayari umeiwekea flash/memory card ulinzi.Kabla haujachomoa flash jaribu kuweka chochote,kama haitoandika maandishi kama haya hapa chini basi utakuwa umekosea kufwata maelekezo(jaribu)

 

 

UKITAKA KUTOA WRITE PROTECTION KWENYE FLASH/MEMORY CARDI FWATA MAELEKEZO

 

#Fwata maelezo yote kuanzia namba 1 mpaka namba 9 lakini ya nafasi ya kumi hakikisha unabadilisha(KUWA MAKINI SANA) na kuandika, ‘attributes disk clear readonly’ Halafu bonyeza Enter

 

 

Hakikisha inakuwa kama picha hapo juu na chini yake pana maandishi yanayosomeka, ‘Disk attributes Cleared Successfully’

 

Jaribu kuweka chochote kwenye flash/memory card na utaona vitu vinahamishika kama picha inavyoonekana hapo chini.

 

 

Mbinu hii itakusaidia kwa ulinzi wa kuhifadhi vitu vyako na hakuna yeyote atakayeweza kuhamisha pasipo kujua mbinu hii na bila idhini yako.kama umekosea kufanya hvyo hakikisha unatuliza akili na kusoma kwa makini kuhusiana na mbinu hii halafu chukua muda wa peke yako kujaribu tena.

Comments are closed.