The House of Favourite Newspapers

Instagram Sasa Itabidi Ulipie Ili Kuona Maudhui

0

Mtandao maarufu duniani wa Instagram sasa unafanya majaribio ya maboresho ambapo mtumiaji wa mtandao huo sasa ataweza ku-Subscribe na kulipia ili kuweza kuona maudhui kwenye akaunti za watu aliowafuata.

Yaani kwa lugha rahisi, wewe unayesoma hapa itakubidi ulipie kiasi cha fedha kitakachokuwa kimetajwa ili kuona maudhui ya mtu uliyem-follow.

Subscription ya Instagram itamuwezesha mtengeneza maudhui kuweka kiwango cha pesa akitakacho kwa mwezi ili mtumiaji aweze kuona maudhui yake.

Gharama za kuona maudhui hayo, mmiliki wa akaunti anaweza ku-set kuazia Senti 99 hadi USD 99.99 ambazo ni sawa na TSh. 230,000 kwa mwezi.

Huduma hii imeletwa mahsusi na Instagram ili kuwasaidia watengeneza maudhui kujiingizia vipato. Ni baada ya mtandao huo kuanzisha subscription kwa watumiaji wa Facebook ambayo imeonekana kufanya vizuri sokoni.

Subscriber Lives: Watengeneza maudhui wataweza kurusha exclusive Lives kwa wateja wao walio-subscribe, na kuwaruhusu ku-engage zaidi.

Subscriber Stories: Watengeneza maudhui wataweza kutengeneza stories maalum kwa subscribers wao, kuruhusu ku-share maudhui ku-exclusive.

Subscriber Badges: Watengeneza maudhui wataweza kuruhusu subscribers wao ku-comment na kuwatambua kwa urahisi.

Leave A Reply