The House of Favourite Newspapers

Jiji Concert Kutikisa Dar Live

0

UNAAMBIWA historia itaandikwa na jiji litasimama kwa saa 24, pale ambapo jukwa la kimataifa la kupanda na kushuka lilipo Kiwanja cha Taifa cha Burudani, Dar Live jijini Dar litakapobeba kijiji cha wasanii kupitia Tamasha la Jiji Concert litakalofanyika Agosti 22, mwaka huu.

 

Jiji Concert ni tamasha la kihisitoria lililoandaliwa na Kandoro Baba kwa kushirikiana na Dar Live likiwa na lengo la kutoa kila aina ya ladha ya muziki unaotikisa Bongo kama Bongo Fleva, Hip Hop, Taarab, Mchiriku, Singeli, Matarumbeta na ladha zote za Kiafrika.

 

Vichwa vikali kama Bright, Tunda Man, Baba Levo, Recho Kizunguzungu, Msaga Sumu, Mzee wa Bwax, Man Fongo, Mimah, Tamimu, Dogo Balaa na wengine kibao watapishana stejini.

 

Kwenye Taarab na matarumbeta atatikisa Rahma na Kiroboto OG, huku wazee wa Mchiriku wakiwakilishwa na sela lao, Machupa Baba. Vurugu zote hizo zikihusishwa kwa mtonyo wa buku tano tu, pale mlangoni.

Unaambiwa kuwa, kuna VVIP ambayo itakuwa maalum kwa ajili ya huduma za kipekee ambapo watu watakaokaa eneo hilo watahudumiwa na watoto wakali wenye majina mjini.

 

Akizungumzia tamasha hilo, meneja Kandoro alisema: “Tumekuja na Jiji Concert kwa lengo la kuwapa watu kifurushi cha burudani katika jukwaa moja. Unajua hili jiji ni kubwa sana, lakini sisi tutalifinyafinya na kulidondosha pala Dar Live, Mbagala.”

 

Unaambiwa mambo yatakuwa mengi kuliko muda wenyewe. Vuta picha unagonga bia, halafu Jike Shupa anakukanda mgongo au unakula nyama choma huku Masha Love ‘Don Dada’, akikubusu shavuni?

 

Itakuwa burudani siyo? Basi huduma hiyo ya kipekee itapatikana kwa mtonyo wa shilingi 50,000 na utakaa Ki-VViP kweli, hii inaitwa ushindwe mwenyewe, wanasema usikose pale Dar Live.

STORI: ISSA LIPONDA

Leave A Reply