The House of Favourite Newspapers

Jiji Concert Wasanii Walivyoshindana Kuonesha Mavituz Dar Live

0
Mfalme wa uswazi, Msagasumu

Ile shoo ya Jiji Concert iliyosubiriwa kwa hamu usiku wa kuamkia leo ilifanyika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live ambapo wasanii kibao walipanda stejini kufanya yao.

Man Fongo alivyokamua.

Miongoni mwa waliokamua stejini ni wakali wa singeli Msagasumu, Man Fongo, Mfalme Ninja Mac Zube na wengineo.

mashabiki wakijimwaya kwa raha zao.

Mambo hayakuishia hapo wapenzi wa mipasho walinogeshwa na Aisha Othaman wa Kundi la Vuvuzela Classic.

Aisha Othaman wa Vuvuzela Classic Modern Taarab akifanya yake.

Recho Kizunguzungu naye alipanda stejini na kuonesha ukali wake kwenye Bongo Flava kwa kuwachizisha jamaa na nyimbo zake zilizoshiba mashairi ya kimahaba.

Recho akikamua jukwaani.

Shoo hiyo ilipigwa mpaka majogoo hivyo kuwafanya mashabiki kuruka mwanzo mwisho.

Recho akimchagiza shabiki kwenye shoo hiyo.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply