The House of Favourite Newspapers

Jike Shupa afanya pati ya aibu

0

Nuh (2)Stori: GLADNESS MALLYA NA

GABRIEL NG’OSHA, WIKIENDA

Dar es Salaam: Muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah al­maarufu Jike Shupa, amefanya pati ya aibu na kuzua minong’ono kwa baadhi ya wahudhuriaji.

Pati hiyo ya ‘bethidei’ yake ilichukua nafasi Siku ya Idd Pili ndani ya Hoteli ya Mambo Sasa iliyopo Sinza, Dar ambapo kulikuwa na watu mbalimbali wakiwemo ‘wanaume tata’ licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwatangazia vita.

Wikienda, likiwa ndani ya nyumba, lilimshuhudia Jike Shupa akiwa amekolea kwa ulabu ambapo ulipofika muda wa kukata keki ndipo akaonesha vituko akiwalisha marafiki zake lakini alipofika kwa mwanaume ambaye anadai ndiye mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la Max, alitulia kidogo na kumlisha kwa mdomo (njiwa staili).

Wawili hao waligandana kwa dakika kadhaa wakiwa ‘wanadendeka’, hali iliyosababisha baadhi ya watu kupigwa na butwaa huku wakinong’onezana kuwa siyo vizuri kufanya mambo ya chumbani hadharani bila tone la aibu.

“Kiukweli hii ni pati ya aibu, hebu angalia wanavyofanya mambo ya faragha hadharani, hawa wasanii wetu wana mambo ya ajabu sana, angalia hata …. (wanaume tata) wamekuja hapa na walishapigwa marufuku na mkuu wa mkoa lakini naona bado hawataki kufuata agizo hilo,” walisikika wakijadili baadhi ya wahudhuriaji ambao wengi walikuwa watoto wa mjini.

Hivi karibuni, Jike Shupa alishushiwa kipigo cha aina yake na mpenzi wake aliyetajwa kwa jina moja la Ramsey baada ya kukuta meseji za kimapenzi na picha za Max kwenye simu yake lakini bado hajakoma.

Leave A Reply