The House of Favourite Newspapers

Jike Shupa Atokwa Povu, Kisa Wanaume Tata

Zena Mustapha ‘Jike Shupa’.

MUUZA nyago aliyejipatia umaarufu kupitia Wimbo wa Jike Shupa wa mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, Zena Mustapha ‘Jike Shupa’ amewatolea povu watu wanaomsema kuwa anapenda kuishi na wanaume tata ‘mashoga’.

Akizungumza na Star Mix, Jike Shupa alisema kuwa, ni ajabu kwa mtu kumuandama, kisa amekuwa karibu na mashoga badala ya kuendelea na maisha yake na kutatua shida zake.

 

“Jamani naona watu wananishangaa kuwa karibu na mashoga, lakini wakumbuke kuwa ni watu kama walivyo watu wengine, wala siwezi kuwaacha hata kidogo, endeleeni na maisha yenu niacheni,” aliwaka Jike Shupa.

Stori Na Imelda Mtema, Dar

Comments are closed.