The House of Favourite Newspapers

MWENYEKITI UVCCM APOKELEWA KWA KISHINDO DAR

Mwenyekiti mpya Taifa wa  Umoja wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),Kheri James akizungumza nawaandishi wa habari ukumbi wa Vijana Kinondoni, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala (kushoto) akiteta jambo na Kheri James.
Baadhi ya vijana wa UVCCM waliohudhuria katika hafla hiyo.

 

MWENYEKITI  mpya Taifa wa  Umoja wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James  amepokelewa kwa kishindo na vijana wa UVCCM wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati akitokea mkoani Dodoma.

 

Hafla hiyo  imefanyika jana   katika ukumbi wa Vijana Kinondoni  jijini Dar es Salaam.

Kheri alichaguliwa rasmi kuwa mwenyekiti Desemba 13 mwaka huu katika uchaguzi  uliofanyika mjini Dodoma na kuibuka  mshindi kwa kupata kura 319.

 

Akizungumza mara baada ya mapokezi hayo, Kheri alisema ni wakati wa vijana wa jumuiya hiyo kuwa ngangari katika kupambana na rushwa inayoharibu taswira ya nchi kwani rushwa haijengi bali  itawafanya vijana kuwa wasindikizaji tu katika taifa.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

 

Comments are closed.