The House of Favourite Newspapers

JIKE SHUPA AVUNJA KIAPO

Juma Kassim ‘Nature’LICHA ya kuapa kwamba hatazaa mtoto mwingine zaidi ya yule aliyezaa na mwanamuziki, Juma Kassim ‘Nature’, muuza nyago kwenye video mbalimbali za wasanii wa Bongo Fleva, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amevunja kiapo hicho baada ya kuonekana na ujauzito ‘kitumbo ndii’.

Jike Shuka ameziambia Za Motomoto News baada ya kuhojiwa juu ya imekuwaje kuamua kuvunja kiapo alichoweka ambapo alikiri kuwa alishatoa mimba nyingi hivyo kwa sasa ameamua kumzalia mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Montelego kwani anahitaji mtoto.

“Siku hizi nashindwa kujichanganya kama zamani kwa sababu ya ujauzito na nimeamua kuvunja kiapo na kubeba mimba kwa sababu ninampenda sana mpenzi wangu na ni muda mrefu anahitaji mtoto, nami nimeona nimridhishe nafsi yake,” alisema Jike Shupa.

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.