The House of Favourite Newspapers

NISHA: PENGO LA MAJUTO HALIFUTIKI MAISHANI

Salma Jabu ‘Nisha’

STAA wa filamu za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye alikuwa akiigiza mara kwa mara na aliyekuwa mkongwe wa filamu, marehemu Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ amefunguka ya moyoni kuwa, pengo alilomwachia mzee huyo halitafutika maishani mwake.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Nisha alieleza kuwa, kifo cha Mzee Majuto kimemuumiza kupitia kiasi na pengo alilomwachia moyoni mwake ni kubwa kwani mashabiki wa filamu hasa za vichekesho wasingemjua.

“Mzee Majuto nilikuwa namwita baba kwa sababu amenitoa kisanaa, yaani alikuwa ni kiungo muhimu sana maishani mwangu, machozi na maumivu yangu havitafutika, nashindwa kuamini na pengo lake halifutiki maishani mwangu,” alisema Nisha

Stori: Gladness Mallya, Dar

Comments are closed.