The House of Favourite Newspapers

JIKE SHUPA: Ngoja Nizae Wataisoma Namba


W
ATAISOMA namba! Video queen na muandaaji wa shoo za Vibao-Kata Bongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amesema kwa sasa hasikiki mjini kwa sababu ni mjamzito, lakini akishajifungua watu wataisoma namba.

 

Akizungumza na Over Ze Wekeend juzikati, Jike Shupa alisema kuwa, watu hawasikii purupukushani zake ila akishajifungua, kila mtu atajua ameibuka tena mjini.

 

“Najua mjini kumepoa sana kwa sababu mimi kubwa lao sisikiki, lakini ngoja nizae kwanza, nikikaa sawa, wataisoma namba na vimbwanga vyangu kama kawa,” alisema Jike Shupa ambaye ni mmoja wa warembo wasumbufu mjini.

Na Imelda Mtema

Comments are closed.