The House of Favourite Newspapers

Lynn Anyoosha Mikono Kwa Tanasha

AMEKUBALI yaishe? Video queen wa Bongo Fleva, Irene Hilary ‘Lynn’ amenyoosha mikono na kumtakia kila la heri mpenzi mpya wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Tanasha Donna.

 

Akizungumza na Over Ze Weekend, Lynn ambaye aliwahi kutajwa kuwa mbioni kuolewa na Diamond alisema anawashangaa wanaosema anaumia juu ya kitendo cha Diamond kutangaza kumuoa Tanasha, jambo ambalo si kweli.

“Sina kinyongo, Diamond amuoe Tanasha hata kesho maana ni jambo la heri.

“Ninafurahi sana kwa sababu Diamond ni mshkaji wangu sana na si vinginevyo,” alisema Lynn ambaye kwa sasa amejiingiza kwenye Bongo Fleva.

IMELDA MTEMA

Comments are closed.