The House of Favourite Newspapers

JINI MTU-06

Taarifa za ajali ya wachezaji wa timu ya joy  zilikuwa gumzo karibu nchi nzima, taarifa zilisema gari liltumbukia katika kolongo na kuwaka moto kiasi cha miili yote kutekea kwa moto na kuhalibika vibaya hata kushindwa namna ya kutambua miili ya marehemu..hii iliibua simanzi kila kona ya mji wa Kigoma ulikuwa ni msiba mkubwa mno.

Tukio hili lilileta athali kubwa  kwa familia yako Vegas, mama yako alipata mshituko uliopekea kupooza viungo vyake.

Tangu hapo akawa ni mtu wa kitandani. wadogo zako wawili  wa kike  walihangaika mno katika kumlea mzazi wako kwani walikuwa ni wadogo.

Ikabidi mjomba wako achukue jukumu la kuilea familia nzima, lakini kwa bahati mbaya miezi sita badae mama yako alifariki dunia,.

Maisha yaliendela kuwa magumu kwa wale mabinti wadogo  yanii Rehema na Mwashamba ikapelekea kuingi katika magenge mabovu ilimladi tu kukidhi haja za mahitaji yao. Rehema akawa anauza mwili wake ilimuladi apate sent ya kukidhi mahitaji yake, akawa kahaba mkubwa mjini kila mwanume akamjua  mwishowe akapata maambukizi ya VVU na mwaka mmoja badae akafariki dunia kwa maradhi ya UKIMWI.

Aliye baki alikuwa ni Mwashamba ambaye hadi leo hakuna anae jua yuko mahala gani. Alisema Nasra.

Moyo wangu uligubikwa na simanzi kubwa sikuweza kuyazuai machozi kupenya katika macho yangu nililia kama mtoto mdogo.

Maisha yangu yalikuwa ni fumbo ambalo hadi dakika hiyo sikujua nini maana ya fumbo hilo.

“Ni muda gani umepita tangu hayo yatokee?” niliuliza huku nikihisi akili yangu ikizunguka.

Mambo yote hayo yamechukua takribani miaka nane na ushee, Alisema kwa kwikwi ya kilio.

Nasra alipandisha kamasi na kufuta machozi yaliyo kuwa yakimtoka machoni mwake kisha akendelea kusema,.

“Kama kuna kitu muhimu nilikuwa nimekosa basi ni kukupoteza Vegasi, siku zote ilikuwa ni msiba kwangu, miaka mitatu ilipita lakini taswira ya sura yako ilikuwa ikinijia akilini kila mara, nilishindwa kabisa kukufuta akilini, Kuna wakati nilikuwa nahisi pengine umeenda safari ila siku moja utarejea, moyo wangu haukuwa tayari kabisa kukubali kuwa  wewe umekufa,  lakini miaka ilizidi kupita pasina kukona”

Alisema Nasra, kisha akasita kidogo akatizama angani kama kwamba anakumbuka kitu fulani, machozi yakiendelea kumbubujika, akapandisha kamasi kabla ya kutoa leso na kujifuta matone ya machozi katika macho yake, kisha akaendelea kusema.

“Nikachukua uamuzi wa kuolewa nikiamini utafutika akilini mwangu, nikaolewa na bwana mmoja mswalihina aliyekuwa na kila kitu cha thamani anacho hitaji binadamu kuwa nacho”

Sauti ya Nasra sasa ilikuwa ikiendena na kilio ambacho kilifanya asimulie kwa kusita sita, nilinyoosha mkono na kumgusa bega kama ishara ya kuumpa nguvu.

Alipandisha tena kamasi akakohoa kidogo kisha akaendelea kueleza.

“lakini ndoa ile haikumaliza hata mwaka yule bwana akanipa talaka tatu.” Alisita kidogo ili maneno yale yaniingie vizuri, akiwa bado  anaendelea kunipa maelezo ya matukio yaliyopita. Alisema

“Kila mara nilipokuwa nikikutana kimwili na yule bwana, nilikuwa nikijikuta nikikuita jina lako badala ya lake kwa huba la penzi zito la yule mtu, actualy hakuna mwanaume ambaye atapenda tabia hii lakini jambo ambalo hakulijua yule bwana ni kuwa wewe haukuwa umefutika katika akili yangu.

Ilitokea  mara ya kwanza akanionya,  mara ya pili akanionya tena, ya tatu akiniacha kwa talaka tatu, ilikuwa kama utani, lakini jambo hilo dogo lilivunja kabisa ndoa yangu, sambamba na hayo, bwana yule  hakuniacha hivi hivi,  alinigawia vitu vingi tu ikiwa ni pamoja na gari na nyumba hii ni kwakuwa nilikuwa na ujauzito wake.

Mimba yangu ilipokuwa kubwa niliondoka Kigoma na kuelekea Bulundi kwa shangazi kwa ajili ya kujifungua,

Hata miezi kadhaa kupita  baada ya kujifungua nikiwa katika mizunguko ya huku na kule katika mitaa ndipo nilipo kuona wewe ukiwa ni mwenye wazimu, kichaa, mwehu, mtu uliye changanyikiwa vibaya mno,

Nilitishika sana baada ya kukuona kwani tayari moyo wangu ulishakata tamaana kuamini kabisa kuwa ulifariki.. sasa vipi tena uibuke ugenini ukiwa hai?, ilikuwa ni kitendawili kisicho kuwa na majibu hadi dakika hii.

Pamoja na kufuatilia habari zako kiundani kutoka kwa wenyeji wa Bunjumbura, lakini hapakuwa na mtu mwenye taarifa za uhakika kuwa wewe ulitokea wapi.”

Nasra alimaliza kusimulia.

Pale nilipo kuwa nimesimama niliona sakafu yote inadidimia chini huku mimi nikibakia angani naelea.

Nilihisi kuzunguzungu matukio ya ajabu kabisa nilipitia..Kamasi jembamba lilikuwa likinitoka huku machozi yakimiminika kama maji katika macho yangu.

Sasa ikawa ni zamu ya Nasra kunibembeleza, alinipa maneno mengi ya faraja huku akinitaka na mimi nimweleze kitu gani kilitokea katika maisha yangu.

“Niletee maji ya kunywa,”  nilimwambia Nasra kwani koo lilikuwa limenikauka kwa kilio.. alinyanyuka na kuelekea sebuleni katika jokofu kwa ajili ya maji.

Wakati huo ilikuwa yapata saa tano usiku..

Wakati Nasra anakwenda kuniletea maji ya kunywa.

Mara ghafla…

Nikasikia kishindo kikubwa  huko nje huku milio ya bunduki ikilindima kuja pale nyumbani.

Nikiwa sijapata uimara mzuri wa akili mara nikasikia kishindo kingine kikubwa zaidi katika mlango wa kuingilia mule ndani na hapo hapo nikasikia sauti kali ya hofu kutoka kwa Nasra.

Fikra zangu zikiwa zinahama katika mtiririko wa matukio ya maisha yangu na kwenda  katika ile taharuki iliyo ibuka ghafla pale nyumbani mara hiyo hiyo nikamwona Nasra akiingia ndani kwa kasi mkononi akiwa amembeba mwanae.

Lakini ndani ya Sekunde hiyo hiyo Jamaa wanne wenye Bastola kubwa usoni wakiwa wameziba nyuso zao kwa vitambaa vyeusi na kufanya kuwa na mwonekano kama wa ninja walijitoma ndani kwa kishindo.

UWIIIII MAJAMBAZIII!.” Nasra alibwata kwa sauti ya juu lakini hapo hapo nikaona risasi nyingi mno zikitoka katika midomo ya  bastola za wale jamaa na kutua katika mwili wa Nasra na mtoto wake.

Damu ziliruka.

Nasra akiwa amemkumbatia mtoto wake wakaenda chini kama mzigo hawakutikisika wala kutoa sauti walitulia tuli lakini ajabu wale watu hawakuacha kumimina risasi katika mwili wa Nasra.

Kiasi niliona matundu mengi mno yakitiririsha damu katika mwili wa Nasra na mwanae tayari wakiwa MAITI,  hapo hapo wale jamaa wakatoweka kwa kasi eneo lile huku wakipiga hovyo risasi hewani.

Lilikuwa ni tendo lililotokea   haraka mno,.

Nilibaki nikiwa nimeziba masikio yangu kutokana na milio mikali ya risasi mach o yangu yakiwa yameduwaa katika mwili wa Nasra na mwanae waliokuwa wameloa damu vibaya mno.

Nilihisi Dunia nzima inazunguka huku ikinizomea na kunicheka nilijiona mdogo zaidi ya nukta.

Hivi naota ama ni…ni..haiwezekani  hii ni ndoto hii lakini kwanini naptwa na ndoto mbaya kiasi hiki..sitaki hii ndoto mimi hebu Mungu niamshe katika huu usingizi wenye ndoto mbaya kiasi hiki..nitoe katika ndoto hii…amka vegasi amka”

   Nilichanganyikiwa vibaya mno, nilibwata hovyo,nilipata uwazimu kwa nukta kadhaa mule ndani nikiwa bado nimeduwaa mbele ya miili ya ile.

Kusema ule ukweli sikujua nini kinacho tokea katika maisha yangu.

Sikujua.

Dakika kadhaa watu wengi walifurika mule ndani wakiwemo askari polisi na waandishi wa habari.

Nililia mno Nasra alikuwa amekufa katika wakati ambao nilikuwa namwitaji sana.

Maisha yangu yalikuwa ni Msamiati mgumu mno ambao sikujua nini Tafsri yake na sikuona wa kunipa jibu la tafsi ya msamiati huo.

“Kivipi Nasra afe, kwanini afe katika kipindi hiki ambacho mimi nimerejea? kwanini?” nililia mno peke yangu wakati mwili wa Nasra unaingizwa katika gari la hospitali ya maweni tayari kwa kupelekwa wodi ya maiti.

Nasra alikufa akiwa na shauku ya kujua yale yaliyo nisibu katika maisha yangu.

Sikujua wauwaji wa Nasra na mwanae walikuwa na chuki gani hadi kumua kikatili kiasi kile yeye na mtoto wake na kuniacha mimi nikiwa hai!..

Nilichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi kwa mahojiano, huko kituoni  nilieleza kile ninacho kijua kwa ufasaha kabisa mbele ya askari mweusi mwenye misuli migumu katika mikono yake..

“Umesema wewe na marehemu mlikuwa na siku ya pili toka mtengane kwa miaka saba siyo?” aliuliza yule polisi mpelelezi akinitumbulia macho yake mekundu.

“Ndiyo afande nilijibu huku nikitikisa na kichwa kwa msisitizo zaidi.”

“Na umesema ulipatwa na ugojwa wa akili kwa mika mingi ukawa mwehu wa mitaani?”

Aliuliza tena yule afande huku akinitizama kwa makini zaidi.

Nilitikisa kichwa tena kumkubalia.

“Unafikiri kwanini wauaji walimua Nasra peke yake na mtoto wake huku wakikuacha wewe ukiwa mzima?.”

“Hilo ndio na mimi linanichangaya afande.”

Yule askari aliuma meno yake huku akiwa anatafakari kitu mishipa ya kichwa ikiwa imemsimama, kisha akanitupia swali jingine ambalo nilishindwa kabisa kulijibu..Alisema “una uhakika gani kama kweli Nasra alikuwa ameachana na mume wake kweli?”

“Aaagh..sina uthibitisho mwingine mbali na kauli ya Nasra mwenyewe aliye nieleza hayo..?”

“Kuwa ameachana na mumewe?”

“Ndiyo afande”

“Okey  vizuri..” alisema yule askari akasimama na kunisogelea katika kiti nilicho kuwa nimekalia kisha akiniuliza huku akiwa ananitizama kwa jicho kali la chuki..

“Unaweza kuniambia   Ashimu Azizi ni nani?

“Nini?”

‘Nini’ ndio nini? Nimekuuliza unaweza kunieleza Ashimu Azizi ni nani”? aliniuliza kwa ukali.

“Ashimu Azizi?…Ndio nani jina geni simjui huyo mtu.”Nilisema nikiwa sielewi maana ya swali lile kwa yule askari mwenye lafudhi ya kiswahili kama cha wenyeji wa mkoa wa Mara, iliyokuwa na shuruti zaidi.

“Humjui huyo mtu? Na jina lake ni geni siyo? Hata huu mpango pia ni mgeni kwako?”

Alisema huku akinitupia kipande cha karatasi kilicho kuwa na mandishi yaliyo someka hivi;

   Hizo ni salamu zangu kwako,na huo ni mwanzo tu bwana Vegas,haikuwa ujanja wewe kukimbia na  cocaine zangu zenye thamani zaidi ya milioni mia na sitini,naamini sasa unaona maimivu ya kuondokewa mke na mtoto.nimefanya kama ulivyo fanya kwangu kwa mauwaji ya mke wangu na mtoto,.huo ni mwanzo tu mchezo bado unaendelea,.

   Hashimu Azizi.

“Whaaaat! hii mimi sijui chochote mkuu” nilisema huku nikimtizama yule askari kwa fadhaa kuliko mshangao.

Afande hakusema kitu wala kujishughulisha na mimi alimwita kosntebo na kumuamulu aniingize ‘lockup’

“NO NO NO hii hainihusu mimi afande… huu ujumbe umekosewa huu..” nililalama wakati nanyanyuliwa kwa nguvu na yule Konstebo na kuondolewa katika ile ofisi ya yule askari mpelelezi.

Nilijiona ni mtu mwenye mkosi mkubwa katika ulimwengu,nilihisi labda nina laana katika maisha yangu,.Nusu ya masha yangu ya ujana yalitawaliwa na misuko suko mikubwa kabisa.

Nikiwa selo nililia mno, nilikuwa na msiba mkubwa katika moyo wangu, kwanza msiba wa mama yangu na mdogo wangu, pili msiba wa Nasra na mtoto wake, tatu msiba dhidi ya maisha yangu ambayo yaliingiliwa na vitu vya ajabu kabisa visivyo eleweka japo kubwa lililo tanda katika roho yangu kwa dakika ile ni  ni kifo cha Nasra.

Bado moyo wangu haukuwa tayari kukubali kama Nasra amefariki dunia.

  “Nasra umekuja maishani mwangu kama Malaika  wa ukombozi wakati nikiwa kwenye kizingiti cha umauti katika nchi ngeni, wewe ukanivuta upande wa uhai na kuniweka mbali na umauti,ukapambana na changamoto za kila aina hadi kufanikiwa kurejesha fahamu zangu,kumbe umejiingiza katika matatizo yangu na kuwawa wewe na mwanao., ona nimekuponza  

Nililia kwa uchungu mule lockup nikibububujikwa na machozi kama mtoto niliketi ukingoni mwa geti la ile selo ya polisi ikiwa kama kwamba akili yangu imesimama kufanya kazi kwa muda, nilibaki katika hali kwa muda mrefu nikibubujikwa na machozi.

Mwisho nilipitisha wazo moja, sikutaka kuendelea kusononesha nafsi yangu kwa kuwa na mikosi katika maisha yangu kwani kama kulia nishalia vya kutosha sasa ilikuwa ni wakti wa kuyapatia ufumbuzi kiini cha mikosi kuandama maisha yangu,.

Wakati huo huo geti la selo lilifunguliwa nikaamriwa kutoka mbele ya askari mnene mfupi mwenye tumbo kubwa lililotokeza kwa mbele almaarufu kama ‘kitambi’.

“Kuja wewe zungu la unga leta mwili wako upesi huku” aliniita jina lililo niongezea hasira moyoni.

Niilitolewa na yule askari mfupi na kutiwa pingu katika mikono yangu kisha nikapelekwa katika chumba kilicho kuwa na uwazi mkubwa huku katikati ya chumba hiko kukiwa na viti meza iliyo zungukwa na viti viwili, nikaamriwa kuketi katika kiti kilicho kuwa nyuma ya meza huku juu yaku kukiwa na barbu ndogo ya umeme iliyo nimulika kwa ukaribu hadi nikawa nahisi joto.

Punde waliingia askari wengi mule ndani wakiwa wameongozana na watu wengine wanne waliokuwa wamevaa kiraia huku katika wale watu wanne mmoja wao alikuwa na asili ya Asia walikuwa wamevaa suti nzuri za rangi ya kijivu.

lile kundi la watu wanne walipo pata kuingia mule ndani yule askari mwenye kitambi alitoa saluti akiwa amekakamaa kwa heshima kisha akasogea pembeni kuwapisha wale watu ili nionekane vema mbele yao.

Wale watu wanne walinitizama kwa kina huku wakiwa wananongo’na taratibu kama kwamba wanelekezana jambo dhidi yangu.

PIA katika lile kundi la watu wanne palikuwa na askari mwingine mnene mrefu aliyekuwa amevaa mavazi ya kipolisi huku katika babega yake kukiwa na mkanda uliozunguka sawa na kiuno chake huku katika bega la nguo yake kulikuwa na nyota nyingi, nikaelewa alikuwa ni mkuu wa polisi,  japo sikujua alikuwa ni mkuu wa ngazi gani.

“Askari hebu tokeni nje kwanza wote, yahitajika tufanye mazungumzo na huyu mtu kwanza.” Alisema yule askari ambaye alionekana kama kiongozi wa maaskari wote,

Askari wote walisaluti kwa heshima kubwa kisha wakatoka nje, mule ndani wakabaki wale watu wanne na yule askari mkuu.

Moyo wangu ulipata usugu wa hofu, sikuwa na hofu na lolote japo hali ilivyo onyesha kesi iliyokuwa mbele yangu ilikuwa kubwa mno na nikesi iliyo gusa hisia za watu wengi.

“jina lako?” askari mkuu aliuliza akiwa amekamata kifimbo cha kipolisi mkononi mwake.

“Vegasi”

“Vegasi hukuzaliwa na baba wewe?” aliniuliza kwa dhihaka.

“ooh marafiki walikuwa wananiita hivyo,naitwa..aah..Jina langu naitwa Kassim Mbwana, lakini hiyo ilikuwa zamani sana siku hizi naitwa Vegasi Mbwana”

“Sasa hapa unaona kuna rafiki zako..ama wahuni wenzio wa huko mitaani mnaouziana madawa ya kulevya na bange hadi mnafanya mauwaji ya watu wasiyo kuwa na hatia..eeh? halafu mtundu sana wewe.”

“Samahani afande..lakini mimi sihusiki na biashara hizi wala sijui lolote juu ya madawa ya kulevya hata kuyaona sijawahi kuyaona..”

Nilijibu kwa mahamaniko makubwa, lakini yule afande  hakuonyesha kuguswa na kauli yangu hata tone.

“Hashimu Azizi ndio nani na anapatikana wapi?” aliuliza tena yule afande huku akiwa amenikazia macho.

“Nijibu mara ngapi swali hilo kuwa mimi simjui huyo mtu”

“Alaa, Unamtetea muuwaji sasa? haya mashtaka yote mawili yatakukabili kijana usipo kuwa makini, mauwaji na uzaaji wa madawa ya kulevya yote mawili utahusika nayo”

Kukawa na ukimya kidogo wale watu wakawa wananongo’na pembeni pasina mimi kusikia lolote.

“Your short life history please?” Alisema jamaa mwenye asili ya Asia akiwa na suti nadhifu ya kijivu usoni akiwa na miwani ndogo ya macho iliyo mkaa vema, sura yake haikuwa ngeni machoni kwangu kama kuna mahala niliwahi kumwona lakini sikukumbuka ni mahala gani nilipo mwona yule Muhindi.

“Tueleze maisha yako kwa ufupi wewe Kassim sijui nani vile Vegas.!” Alisema yule afande katika namna ya kunitafsilia yale maneno ya kingereza ya yule muhindi ambayo siyo kwamba sikuyaelewa.

“Nilifahamika kama Vegasi, ni mtoto wa kwanza kati ya watatu, mkazi wa hapa hapa Kigoma,Elimu yangu ni kidato cha sita, ni hayo tu wakuu”

Nilisema,niliona tena wale watu wananongo’ona kama kuna kitu walitaka kukijua kutoka kwangu lakini hawakukisika,Walinitizama kwa kina huku nikiona tafakuli ya kila mmoja machoni pake juu yangu,

“Unafanya kazi gani wewe?” aliuliza mtu mwingine mweupe mnene kimwonekano akiwa ni mtu tajiri asiye na dhiki  hata kidogo.,

“Sina kazi wakuu”

“Sasa unaishi vipi?”

“Nilikuwa mgonjwa katika kipindi kirefu mno nilipatwa na wazimu wa akili kabla ya kupoteza fahamu katika kipindi kingine kirefu mno”

“Umeanza kutumia madawa ya kulevya muda gani?” alidakia yule afande akauliza swali ambalo liliniudhi moyoni

  Kwanini sieleweki kwa hawa maafande jama.

“Jamani niseme mara ngapi tena kuwa, mimi hayo madawa hata kuyaona sijawahi kuyaona, sasa vipi niwe mtumiaji ama sijui muuzaji wa hizo biashara?” Nilijibu kwa kulalamika japo hakuna aliye onekana kuguswa na mahaminiko yangu.

“Ilikuwaje ukawa na wazimu?” aliuliza jamaa mwingine ambaye alikuwa kimya muda mwingi.

“Ni habari ndefu mno ila kwa ufupi tu, mimi ni muhanga wa ajali ya basi lililotokea miaka saba iliyopita ambalo lilikuwa limebeba wachezaji wa timu ya Joy football club,nilipatwa na masaibu makubwa mno ya kichawi kwani kwa macho yangu niliona wachezaji wenzangu wakiliwa nyama ilihali wakiwa wazima na viumbe wa ajabu,..sijui nini vile mashetani ama nafikili majini..ni mimi peke yangu niliye fanikiwa kutoroka huko tulipokuwa na kujikuta nimepatwa na wazimu kwa miaka mingi kabla ya kupata msaada kwa Nasra binti ambaye nashutumiwa kuwa nimesababisha kifo chake” nilisema.

Wale watu watatu waliovaa suti za kijivu walionekana kuingiwa vema na maneno yangu, tofauti kidogo kwa yule afande ambaye mara zote alinichukulia kama teja niliye pagawa kwa madawa ya kulevya,.

“Wewe hebu ondoa upuuzi wako hapa wa kijinga sema Ashimu Azizi ni nani..wee mtoto jua hapa unaongea na waziri.” alisema huku akielekeza kidole kwa yule jamaa mrefu mweupe mwenye kunukia pesa, “na siyo waziri tu, elewa kuwa unazungumza na mkuu wa polisi mkoa  vilevile unaongea na mkuu wa mkoa”. akomulekezea kidole yule muhindi “pia mkuu wa wilaya,.kwahiyo kuwa makini na siyo hadithi za kijinga unazo leta hapa”

“lakini afande..”

“Shut up blood Coward!” alinikatisha huku akinitishia kunipiga kwa lile lungu lake alilokuwa amekamatia mkononi.

Walinong’ona kwa muda kisha wakaondoka mule ndani, punde baada ya kuondoka wakaingia askari wanne na kunizunguka katika ile meza,

“Vegasi” aliniita askari mmoja katika wale wanne walionizunguka mahala pale.

“Naam Afande”

“Hapa tunagawana kazi kidogo kati yetu na wewe okey?” nilitikisa kichwa kukubali.

“Vema..sasa iko hivi, sisi tutakuwa wauliza maswali na wewe utakuwa mjibuji maswali tena siyo majibu tu, bali majibu sahihi sawa?”

“Sawa afande”

“Na hatutegemei utuletee Riwaya za akina Hamie Rajabu oright?”

“Ndio mkuu”

“Safi sana kijana., sasa tunanaza na swali la msingi kwanza, Ashimu Azizi ni nani?” Aliuliza kwa sauti ya chini yenye kunong’ona lakini yenye shuruti kubwa ya kipolisi

“Jamani mimi nijieleze vipi kwenu kwamba huyo mtu mimi simjui” nilisema huku nikifanya sauti yangu kuwa ya huruma zaidi.

“Aaagh ngoja kwanza tukuonyeshe kwamba tuko sirous na maswali yetu na tunataka majibu sahihi kutoka kwako”

Alisema askari mwingine na kunisogelea na kunivua shati langu kisha akatoa kifaa chenye ncha kali kilicho fanana na vifaa vitumikavyo kucholea duara{bikari}, kisha akinichoma na kile kifaa katika paja langu,akaingiza kwa ndani urefu wa nchi mbili,  “AAAAAHG”  nilipiga makelele ya nguvu maumivu makali yakitambaa katika mwili wangu huku damu zikichuruzika vibaya mno, akazidi kudidimiza ile bikari kwa ndani zaidi hadi nikahisi mapigo ya moyo yanabadilika kwa uchungu wa maumivu, kisha akachomoa huku akitikisa tikisa kulia na kushoto kile kifaa kikiwa ndani ya nyama ya mwili wangu, kisha akachomoa na kubaki tundu dogo lenye kutiririsha damu kwa kasi.

“UUUUUWIIII” nilipiga makelele ya uchungu maumivu yasiyo mithilika yalitambaa katika mwili wangu kisha yule askari alitoa chumvi ya unga katika mkoba wake na kunyunyuzia ile chumvi katika lile jeraha, maumivu yaliongezeka mara mbili zaidi,nilihisi roho inanichomoka,

“Sema upesi WEWE MTOTO…Ashimu Azizi ni nani wewe eeh?”

“Simjui huyo mtu jama..aagh! sijui mimi..mnataka niseme kitu gani ninyi watu?” nililalama.

Yule askari alinitoboa tena katika paja la kulia, akachomoa kisha akinitoboa tena, akachomoa kisha akinitoboa tena huku akinipiga ngumi kali ya pua na kunipasua vibaya katika mgongo wa pua.

“Utazungumza tu mende wewe,.” Alisema afande, mapaja yangu yote yakiwa na matobo mengi yaliyo churuzisha damu nyingi mno, akili yangu ilizunguka kwani nilijikuta napatwa na kimuhemuhe, alichukua ile chumvi ya unga na kuichanganya na unga mwingine mwekundu kisha akanipaka katika majeraha yangu yote ya mwilini.

“UUUUUUWIIIIIIIII”

Nilipiga mikelele ya nguvu yule askari mtesaji alikuwa amenipaka chumvi aliyo changanya na pilipili ya unga..

“Haya sema upesi, Ashimu Azizi ni nani?” Aliuliza yule polisi, nilitamani nimtukanane yule mtu lakini sikuona tusi litakalo mfaa ili liendane na kile anacho nitendea.

“Ok ok…ntasema…ntasema…ni nani…huyo mtu..ntasema” nilisema kwa tabu,nikaona wale polisi wakijiweka sawa kusikia nini nitasema.

“Sogea….tafadhali” nilizungumza nikionyesha niko katika hali mbaya huku nikimtaka yule polisi mtesaji asogeze sikio lake ili nieleze kile walicho taka niseme.

Yule polisi mtesaji akasogeza sikio lake mkabala na mdomo wangu, akiwa tayari kusikia nasema Ashim Azizi ni nani.

Lilikuwa kosa.

Nilimrukia kwa kasi huku nikiunguruma kwa ghadhabu kali kisha nikamng’ata sikio lake kwa nguvu sana hadi nikatoka na pande kubwa la nyama ya sikio,yule polisi alipiga yowe la uchungu na mstuko mkubwa, lilikuwa ni tendo ambalo halikutarajiwa na wale askari polisi hata kidogo.

Hapo hapo nilihisi nikipigwa na kitu kizito katika kichwa changu na kusababisha maumivu makali  yakitambaa katika kichwa changu  maumivu yaliyo pelekea kumuachia yule polisi.

Nikajikuta nashambuliwa kwa kipigo cha hali juu kutoka kwa wale polisi, yule polisi niliye mng’ata sikio aliibuka kama mbogo aliye jeruhiwa  alinibamiza teke kali la tumbo lilio nitupa sentimita kadhaa huku nikihisi pumzi zikibana kutoka,

Nilimtizama yule polisi kwa jicho la chuki, akiwa anatiririkwa damu nyingi katika sikio lake lilio chafua uso wake kwa damu nyingi.

Alinijia huku akiwa anaunguruma kwa ghadhabu kubwa macho yake yakiwa na hasira kali juu yangu alinibamiza teke jingine kali la sehemu zangu za siri, vile nilvyo jisikia ni siri yangu, kwanza nilihisi amenipasua korodani zangu kwani mwili wote uliisha nguvu maumivu makali kabisa sehemu za siri na tumboni yakinisulubu vibaya mno nilihisi nimelowekwa katika chungu cha moto, niliona giza machoni pangu sikujua kilicho endelea tena.

 

Je, nini kitaendelea?

Tukutane kesho hapahapa.

Comments are closed.