The House of Favourite Newspapers

CRDB Bank Foundation, UNDP Kuwezesha Wajasiriamali Wanawake na Vijana

0
*CRDB Bank Foundation, UNDP kuwezesha wajasiriamali wanawake na vijana kunufaika na fursa za AfCFTA*
Taasisi yetu ya CRDB Bank Foundation leo imesaini mkataba wa ushirikiano wa miaka 5 na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) katika maeneo yafuatayo;
✅ Uwezeshaji wa vijana na wanawake, uwezeshaji wa biashara changa
✅ Ufadhili wa miradi endelevu
✅ Utekelezaji wa program za pamoja za kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
✅ Na kushirikiana kwa utaalam maalum na msaada wa kiufundi.
Katika kuanza utekelezaji wa mkataba huo, CRDB Bank Foundation na UNDP wametangaza utekelezaji wa program maalum ya uwezeshaji wa biashara ndogo ndogo na za kati za wanawake na vijana kunufaika na fursa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).
Katika ushirikiano huo utakaodumu kwa kipindi cha miaka mitano, CRDB Bank Foundation itakuwa na jukumu la kutoa elimu ya fedha, mafunzo ya usimamizi na uendeshaji biashara, na jinsi ya kuyaendea masoko ya kimataifa na kunufaika na AfCFTA.
Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP nchini, Shigeki Komatsubara makao makuu ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salaam.
#CRDBBankFoundation
#UNDP
#UbiawaKimkakati
Leave A Reply