JINI MTU-09

Ghafla..

Nilistuka kutoka katika usingizi ilikuwa ni saa kumi na mbili asabuhi ndani ya gereza la bangwe, nilijinyanyua mahala pale nilipo lala katika kigodolo cha futi tatu watu wanne, nikatizama huku na kule..baadhi ya wafungwa na mahabusu walikuwa wamekwisha amka wengine wakiimba nyimbo za dini, huku wengine wakisali, wengine wakijikuna miwasho ya chawa na kunguni katika miili yao, huku wengine wakiwa wametulia wakiwaza matatizo yao, basi ikawa ni kila mtu anafanya yake ambayo akili yake ilimtuma kufanya.

Nilijitizama katika mwili wangu nilikuwa nimetapakaa michanga ya ufukweni na maji kwa hakika akili yangu ilisadaki kabisa kuwa nikilala nakuwa katika ulimwengu mwingine na ninafanya matukio ya ukweli kabisa.

   Mimi ni jini,? Mimi ni machawi? Ama mimi ni mzimu? Mimi nitakuwa ni nani mimi?

Nilijiogopa.

Ndio kusema nimemfufua Nasra..na eti akae siku sita bila kula samaki wala nyama pia asiingiliwe kimwili ndio apate uhai kamili,.vinginevyo..ANAKUFA TENA..

Niliwaza nikiwa nimekusanya miguu yangu na karibu na kifua changu na kujikunyata, nilizama katika bahali ya mawazo.

Saa moja kengele ilipigwa na wafungwa wote katika mabweni tukajianda kwa ajili ya kutoka nje, tulitolewa nje na kuzagaa katika wigo mpana tukiota jua la asubuhi muda mwingi ukitakiwa kukaa chini badala ya kusimama simama hovyo katika wigo wa gereza.

Kulikuwa na ubabe mno ndani ya gereza manyampala ndio walikuwa vilanja wa wafungwa na mahabusu katika gereza, angeweza kukuchalaza viboko ama kukupiga makonzi kama akitaka kufanya hivyo hata kama hujafanya kosa lolote, na hakuna mtu wa kuuliza hilo.

Binafsi nilikuwa mpole mithili ya njiwa, hakuna aliye kuwa akinifahamu katika lile gereza lililosheheni aina kubwa ya wahalifu wenye makosa ya kutisha kabisa.

Katika wigo ule katikati kulikuwa na mti mkubwa wa mchongoma ambapo ilipo timu saa sita jua lilipata kuwa kali na kivuli cha mti huo ndio kilitumika kwa wafungwa kujipumzisha.

Nilikuwa miongoni mwa mahabusu watulivu mno,niliketi chini ya mti huo akili yangu ikiwa maili nyingi, sauti za kiwendawazimu za Nasra huko mtani zilipenya vema masikioni mwangu, alikuwa akiimba nyimbo za kitoto, akicheka cheka hovyo, mara alilia pasina sababu, pia alikuwa akipiga mayowe ya kukimbizwa na mashetani na kufanya watu wamtusi huku wengine wakimpolomoshea maneno ya kejeli kwa vitendo vile alivyo kuwa akivifanya bila shaka ikiwa ni katika ya halaiki ya watu..

Chochote kilicho sikika katika masikio ya Nasra mimi pia niliweza kukusikia nilisikia mazungumzo ya watu walio kuwa karibu yake.

Niliendelea kutulia pale katika kivuli ndani ya gereza fikra zangu zikiwa maili nyingi kabisa, japo sikuona kilicho kuwa cha muhimu katika matendo aliyo kuwa akiyafanya Nasra huko mtaani lakini moyo wangu haukuwa tayari kabisa kuwa mbali na binti yule niliye mpenda mno.

   Njaa,.mimi njaaaaah! nilimsikia Nasra akiongea katika namna ya kiwehu wehu,. na mara hiyo hiyo niikasikia sauti za wanaume ambao bila shaka walikuwa jirani na mahala alikokuwa huko mtaani..

   Ebwana huyu demu mkali ila mbovu wa akili kweli mungu hakupi vyote

   Kweli man Mungu hakupi vyote,hivi unafikili huyu she angekuwa mzima wa akili nani ambaye asinge hitaji kumwoa na kumweka ndani

   Hakuna

NJAAAAAA.. hapo hapo sauti ya Nasra alikuwa akilia iliingia masikioni mwangu na kutosikia tena mazungumzo ya wale watu.

Kweli alikuwa ananjaaa kwani toka nimfufue ule usiku kutoka katika usingizi wa kifo hakuwa amepata kuweka chochote.

Tulia Nasra utakula muda si mrefu nililipeleka wazo kutokea pale nilipo kuwa hadi katika kichwa cha Nasra maili nyingi kutoka kwangu.

sitaki,…nataka kula.. alisema kutokea kule na sauti yake ikasikika masikioni mwangu.

Nilifikili kwa muda,sikuwa na njia ya kumsaidia yule mwanmke huko mtaani aliko kuwa bila ya kulala usingizi na kuingia katika ndoto itakayo niwezesaha kumtokea mahala aliko na kumpa msaada.

Kwa mujibu wa jua ilikuwa ni kati ya saa sita kuelekea saa saba mchana dakika chache kabla ya kengele ya kupata chakula cha mchana kugongwa.

‘Njaaa’ Nasra alizidi kulalama hovyo mitaani,sasa nilisikia kwikwi za kilio kutoka kwa Nasra, neno njaa lilikuwa kiitikio cha wimbo.

Uchungu ulinishika lakini sikuwa na namna ya kufanya zaidi ya kusubiri, tukio la chakula lipite kisha nijilaze walau dakika kumi na tano za kuingia katika njozi kisha nimsaidie Nasra.

Dakika kumi badae kengele ya chakula ilipigwa na wafungwa na mahabusu wote tulipanga foleni kwa kugawiwa chakula, nilikuwa mtu wa mwanzoni kabisa kupewa chakula, nilichukua kile chakula na kutafuta eneo zuri kidogo na kuketi, nilitupa macho yangu pembeni yangu alikuwa ameketi  mzee mmoja miaka kati ya  hamsini.

Alikuwa amekondeana macho yamezama kwa ndani huku ngozi yake ikiwa na vipele vingi na michubuko iliyo tokana na kujikuna hovyo, nilimkumbuka alikuwa ni mtu maarufu mika saba kama siyo nane iliyopita, umaruufu wake ulikuja kutokana na tuhuma nzito zilizo kuwa zikimkabilia za kujihusisha na ufadhili wa vikundi vya kigaidi ambavyo vilileta maafa kwa watu wengi,.

Lakini mbali ya hilo kubwa ambalo lilileta hisia kwa watu wengi kutoka kwake, alikuwa ni shekh mkuu wa musikiti mkuu wa  Kigoma ujiji, taarifa za kesi yake zilikuwa gumzo katika vyombo vingi vya  vya habari miaka hiyo kutokana na  kuhusishwa pia na mipango ya matukio ya mashambulizi ya kigaidi   mjini  Kigoma mwaka 2000 hali iliyo pelekea kuhukumiwa miaka 20 jela.

Huyu si mwingine ni Shekh Othumani hilal

Niliketi pembeni yake  nikiwa na bakuli kubwa lililokuwa na ugali ambao haukupikwa ukaiva pamoja na bakuli la maharage yasiyo ungwa kitunguu wala mafuta.

Nilishambulia kile chakula matonge mawili matatu, lakini hakikupita kabisa katika koo kwani sauti ya Nasra huko mtaani iliyokuwa ikilalama ‘njaa’ ilizidi kunitesa akilini, sikuona raha ya kula ilihali mtu ninae mpenda anateseka kwa njaa.

   Nahitaji nilale mimi niliondoa vyomba kile chakula kikiwa kimebaki.

“Oh oh wewe mwana vipi mbona waludisha,..umashiba?” aliniuliza yule shekh nilipokuwa nimesimama na mabakuli ya chakula tayari kwa kurejesha vyombo.

“Yeah nimeshiba mzee sijisiki kula”

“Unaumwa?”

“Hapana, sina hamu tu ya chakula”

“Hebu acha masikhara wewe kijana,. haya hebu leta huo ugali hapa niustiri, humu ni jela ukiendekeza mawazo utakufa siku siyo zako” Alisema yule shekh, nikampa yale mabakuli ya ugali na maharage, mimi nikarudi kuketi na kulala pale chini..

Dakika tano badae dalili ya kuzama katika usingizi ikawa inaninyemelea, kidogo nikahisi nimeshuhsa  mzigo mzito kwani dakika chache nitakuwa nimeungana na Nasra huko mtaani na tatizo la njaa linalo mkabili nitalipatia ufumbuzi.

Dakika zikazidi kusogea mbele,na mimi nikazidi  kupotelea katika usingizi.

MARA..

Nilistushwa ghafla na sauti kali ya kengele iliyo lilia masikioni mwangu kabisa.

Nilistuka ghafla na kuhisi mapigo ya moyo yakienda kasi.

“Muda wa lokoo kijana”

“Nini?”

Niliuliza nikiwa nimekunja uso kwa fadhaa lakini yule shekh hakunijibu alikusanya kusanya vyombo vyake na kusimama kuelekea katika hilo alilo sema.

‘Lokoo’

Wafungwa na mahabusu wote walikusanyika eneo la wazi na kupanga mistari kwa ajili ya kufanyiwa ‘lokoo’, ambapo badae nilikuja kufahamu kwamba ni kuhesabiwa, huo ulikuwa ni utaratibu wa humo gerezani kila baada ya chakula cha machana wafungwa na mahabusu wote huhesabiwa,{lokoo}

Nilijikuta natukana moyoni utaratibu ule nikiwa na wahka mkubwa wa kumsaidia Nasra.

  Unataka chakula mrembo? Nilisikia sauti za watu huko mtaani zikiongea na Nasra

   Eeeh nataka kula

   Haya njoo huku ule

    Wapi?

   Huku ndani

   Oyaa masela demu anaingia mkenge..akiibuka tu ndani tunasababisha.

   Poa mwana

Nilisikia mazungumzo hayo nikiwa katika foleni ya kuhesabiwa kule gerezani,.

Moyo wangu ulipiga paa, kengele ya hatari ikgonga kichwani mwangu, Nasra alikuwa amechukua wajihi wa  binti mrembo samaki mtu {nguva} hakuna mwanaume ambaye angepata bahati ya kumtizama akaishia kumtizam mara moja.

Wale wahuni ambao nilipata kusikia  wakiteta maili nyingi kupitia masikio ya Nasra ambaye wakati huo akili yake haikuwa inajua lipi zuri lipi baya dalili za kufanyiwa jambo baya ikiwemo kubakwa nililihisi waziwazi.

  Nasra tafadhali naomba uondoke eneo hilo hao watu hawana nia njema na wewe

Nilitupa wazo langu kichwani mwa Nasra, lakini ilikuwa ni kama ninampigia mbuzi gitaa, hakuna alicho jibu Zaidi ya kucheka cheka hovyo.

Nilibaki nikiwa na kimuhemuhe cha hali ya juu, kama Nasra itatokea ataingiliwa kimwili, aidha kula chakula kama samaki ama nyama atakufa jumla kwani atakuwa emekwenda kinyume na taratibu za miungu bahali..

Nilijikuta nikijuta kuto twaa uhai wa wale viumbe  sita wa majini kwa ajili ya uhai wa Nasra, pengine haya yote yasinge tokea nili-ulaumu moyo wangu kwa kuzidiwa nguvu na hali ya huruma ambayo sasa inanighalimu.

Zoezi la kuhesabiwa lilienda taratibu mno kiasi cha kuzidi kuogopa usalama wa Nasra.  Nikatuliza mawazo yangu tena kusikiliza  nini kinaendelea huko Nasra aliko.

Oyaa unakula nini mrembo’

  Chakula’

  Chakula gani?’

  Chakula..’

  Ndio chakula,. ila chakula gani?’

  Chakula..’

  Zimwi eeeh wee unaongea nini na huyu chizi,. wee mchunie hadi tunamwingiza geto then kila mtu anajisevia uroda

Ebwana wee.. nilihisi dunia yote ina zumguka kama kurudumu la baiskeli huku mimi nikiwa kwa ndani,.

Zoezi la kuhesabiwa ndio kwanza lilikuwa linaenda polepole mno, “lazma nifanye kitu.,Nasra anaweza kufa kizembe”

Nikiwa nafikilia nifanye nini mara nilistushwa gafla na sauti kali mno yenye dutu za amri ndani yake ikiniita.

“Vegaaaaaas” niliitika huku tumbo lilikikata kwa hofu.

“Kuja hapa” niliitwa kwa amri kubwa.

Alikuwa ni ofisa mwenye cheo kikubwa kabisa, alinipeleka katika ofisi ya mkuu wa gereza iliyo kuwa ndani ya gereza hilo hilo.

Hata nilipo pata kuingia mule ofsini nilimkuta yule askri polisi wa mwanzoni kabisa aliye fanya mahojiano ya awali na mimi,  hakuwa peke yake alikuwa na mtu mwingine mrefu mwenye kitambi aliye kuwa amekamata gazeti la serikali mkononi,.

Nilistuka nilipo tupa macho yangu katika lile gazeti kulikuwa na picha yangu ndogo na picha ya Nasra kubwa iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti hilo, kulikuwa na mandisi makubwa kabisa yaliyo kolezwa wino mweusi yakisomeka;

   MAITI YA MWANAMKE ALIYE UWAWA KWA KUPIGWA RISASI UMETOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA KUTaTANISHA HOSPITALI YA MAWENI MKOANI KIGOMA.

Chini ya picha ya kubwa ya Nasra kulikuwa na picha  yangu ndogo na maandishi yaliyo kolezwa wino mweusi, yaliyo someka; huyu ni mwanume anae daiwa kuhusika na kifo cha mwanamke huyo ambaye kesi yake anandelea katika Mahakama ya wilaya  Kigoma ujiji.

Nilihisi msisimko wa hofu kidogo kwa kuandikwa katika gazeti, lakini sikuwa na hofu dhidi ya tukio lile, zaidi niliona wale jamaa kama wananipotezea tu muda wa kwenda kumsaidia Nasra ambaye yupo katika hali tete.

“Kaa chini” aliniambia kwa amri yule afisa wa magereza na mimi bila shuruti nikatii.

“Vegasi leo usipo toa jibu zuri la maswali tunayo kuuliza  nakupasua bichwa humu humu gerezani fala wewe”

Alisema yule askari polisi.

Sikujibu kitu kwa  kauli yake kwani sikuona umuhumu wa kushindana na yule mtu ambaye kutokana na uwezo mkubwa niliokuwa nao nilimwona ni mtoto mdogo kabisa anae taka kucheza ngoma asiyo jua inaitwaje.

Hata baada ya kujitambua kuwa mimi siyo mtu wa kawaida nilikuwa nina kiburi na dharau ya kiwango cha juu kwa binadamu wa kawaida.

Yule afande mwenye lafudhi ya kishashi alisogea karibu yangu akiwa na kitabu kidogo cha data na kalamu ya wino kisha akaanza kunihoji.,

“Mwili wa Nasra umeibiwa  kule hospitalini”.

Alisema kisha akinitizama machoni bila shaka kuona ile taarifa yake nitaipokeaje.

Sikuonesha dalili yoyote ya kustuka macho yangu yalikuwa yakitizama pembeni.

Sekunde sita saba zilipita kukiwa na ukimya yule afande akiacha yale maneno yake yaniingie vizuri akilini.

“Unahisi kwanini mwili wa Nasra umeibiwa?. na muhusika wa hili unadhani atakuwa ni nani?”  hatimae aliuliza yule afande ambaye alionekana anaijua vema kazi na kile anacho kifanya, nasema hivi  kwa sababu, niliona umakini wa hali ya juu kwa yule askari polisi namna anavyo soma saikorojia yangu kupitia macho yangu, japo  kitu kimoja tu ambacho hakukujiua.. sikuwa kiumbe wa kawaida.

“Nikikujibu maswali yako   utanisadiki afande?”

Nilimuuliza  ilihali macho yangu yakiwa yanatizama pembeni.

“Jibu unacho ulizwa wewe mtu..na si porojo”. Yule askari mwingine mwenye kitambi alidakia, wakati macho ya yule afande mwenye lafudhi ya kishashi yakiwa makini zaidi kwangu,

“Taratibu afande, kumbuka mimi nilisha kuwa potrayed kwenu kama chizi niliye athirika kwa madawa ya kulevya…sasa  vipi leo mniibukie huku gerezani.?”

Kibao.

Nilikunja uso kwa maumivu huku nikiona nyota mbili mbili.

“Kinacho fanyika hapa ni kinyume na sheria,.mimi na ninyi tulisha malizana tangu huko kituoni sasa vipi tena munisakame  hadi huku gerezani jamani  aaagh”

Kibao tena…

“Pumbavu sheria hiyo aliitunga babu yako..sasa ukijitia kujua zaidi nakutoa ngeo za kichwa ukalale hoi.. pimbi wewe”

Alikoroma yule polisi kwa sauti ya iliyo kwaruza ilihali yule askari mwingine akizidi kunisoma tu.

“Sasa mnataka nini jamani eeh”

“Usijitie uchizi Vegasi umesahau  nilicho kuuuliza” hatimae lafudhi ya kishashi aliuliza kwa hasira.

“Muhusika wa hayo yote ni Hashimu azizi, na ameiba mwili wa Nasra kupoteza aina fulani ya ushahidi ambao ungepelekea yeye kukamatwa.”

“WHAAT?..” Wale askari waliuliza kwa suti kubwa ya pamoja baada ya kusikia majibu yangu.. walipagawa kwa maelezo yangu macho ya yule askari lafudhi ya kishashi yalimtoka pima.

Ni wakati huo huo nilisikia yowe kubwa kichwani mwangu, alikuwa ni Nasra akipiga makelele ya nguvu ya maumivu huko aliko kuwa. “ooh Nasra anabakwa” Nilijikuta nikilopoka kwa sauti, huku macho yangu yakigubikwa na kizungu zungu.

“Unasema…” wale askari waliniuliza kwa pamoja, ikiwa kauli yangu ya awali haija chekechwa vizuri vichwani mwao.

Hapo niligutuka baada ya kugundua nimefanya makosa kwa kauli yangu hii ya pili ambayo nilijikuta nazungumza bila kutarajia.

Nilijikuta moyo wangu unaingia katika wakati mgumu mno  mbele ya wale polisi wawili waliokuwa chemba ya ofisi ya mkuu wa gereza.

    Nifanye kitu gani mimi hapa nilijiuliza nikiwa nimechanganyikiwa mno.

“Wewe mtu kauli zako mbona haizieleweki?”

“Nini ambacho hakijaeleweka hapo afande nimesema muhusika wa yote haya ni Ashimu Azizi. Sasa nini tena jamani,.si mniache mimi niondoke aagh”

Nilisema kwa ukali, nikiona kabisa wale polisi wananitia kiwingu kama siyo kunichelewesha kabisa kwenda kumsaidia Nasra huko mtaani.

Nilikutana na kibao kikali kutoka kwa asakri mwenye kitambi…nilihisi uso mzima ukiwaka moto kwa jinsi maumivu yalivyo nitambaa.

“Unaleta uchizi kwa machizi, ngoja nikuonyeshe uchizi”.

“Nasra akifa huko aliko ujue utakuwa miongoni mwa watakao wajibika na kifo cha Nasra.”

Nilisema kwa kiburi kikubwa kabisa huku nikimtizama yule askari katika namna ya kuchungulia kwa chini kiburi kikiwa kingi machoni mwangu.

Kibao kingine.

“Fala wewe nilisha kukataza jeuli lakini naona husikiii wewe mjinga”

“Wee ndio mjinga afande humwoni mwenzio mwenye akili alivyo mtulivu au usha ahidiwa fungu na Ashim Azizi uje unipige pige huku gerezani?”

Loh! hivi wewe mtoto unajiamini nini?

Lafudhi ya kishashi aliuliza kwa mshangao mkuu.

Kibao tena cha nguvu zaidi..

Dunia nzima niliona inazunguka, nilijishika shavuni mwangu nikahisi alama za vidole vya yule mtu.

“Una..ko..sea sana we..we afande uta..jutia hay unayo yafa….”

Kofi jingine. Lakini hapo hapo nilisikia sauti kali

Maaaamaaaa nakufaaaaaa” ilikuwa ni sauti kali ya Nasra, huko aliko kuwa kukiwa na sauti nyingine za watu wakimkemea kwa sauti ya chini na uficho akae kimya.

Nilibaki nikiwatizama wale maafande wawaili nikiwa sina mbinu ya kitu gani nifanye.

“Ashimu azizi ni nani Vegasi, na kwanini unasema Nasra akifa.! Nasra gani tena akifa wewe?” afande  lafudhi ya kishashi aliuliza kwa sauti tulivu mithili ya mtangazaji wa redio.

“Ni Saumya Kohil,. huyu Mkuu wa wilaya” nilijibu haraka haraka ili walau tumalize lile zogo.

“Niniii!.” Jamaa waliuzia kwa mshangao..

Lafudhi ya Kishashi alinitizama na nikaona hana matumaini na mimi kabisa,

Na huyo Nasra unaesema akifa ni yupi huyo?”  aliuliza kivivu akiwa amekata tamaa kabisa kwangu kwa kuona anaongea na mtu aliyerukwa na akili kwa kiwango kikubwa.

Nilitafakari kwa muda nikapitisha uamuzi mmoja…kuwajibu maswali yao katika namna ya kuwachanganya hivyo hivyo.

“Kwani hapa tunamuongelea Nasra gani afande?”

Kibao kwa mara nyingine tena.

“Nilisha kueleza ukitoa majibu ya kichizi chizi na mimi nakuonyesha uchizi, kisonoko wewe,.wewe ni mjibu maswali tu na siyo mhoji maswali” alisema yule askari mwenye kitambi anaye nisulubu kwa makofi tu.

“Wee nipige tu lakini tendo hili utalijutia.”

Nilipomaliza tu kauli yangu nikakutana na kibao kingine cha uso kilicho pasua kabisa mdomo wangu..niliona ukungu mbele yangu.

“Okey Vegasi, calm down, sasa kama ni  Nasra huyu,.. huyu mtu  Alisha kufa na mwili wake ulio hifadhiwa katika hospitali ya maweni umepotea Vegasi… thus  tuko hapa ili utueleleze walau kile unachoweza kukijua., sasa vpi useme tena,. ‘Nasra akifa huko aliko ujue utakuwa miongoni mwa watakao wajibika na kifo cha Nasra,.  how come this Vegas?”

“Ninacho kiamini mimi Nasra hajafa na kama hajafa maana yake  yupo mahali  fulani anishi japo sijui ni wapi,.kuhusu kutoweka katika hospitali hilo analijua Hashim Azizi, au saumya kohil au kwa nanmna nyingine  mkuu wa wilaya wa walaya hii”

“Kweli wewe unastahili makofi, fala wewe”  Alisema Lafudhi ya kishashi kwa hasira baada ya maelezo yangu..

Kilicho fuata hapo yule askari makini mwenye lafudhi ya kishashi aliondoka ndani nikabaki mimi na askari mwenye kitambi, aliniuliza maswali mengi ambayo kila nilivyo mjibi nilikuta na makofi makali mno katika uso wangu.

Yule mtu aliniuliza mengi kuhusu Ashimu Azizi ajabu kadri nilivyo zidi kumpa majibu kuhusu Ashimu Azizi  ndivyo alizidi kuchanganyikiwa na kufanya maswali mengi dhidi yangu, huku makofi makali ya yule afande yalinifanya nizidi kupoteza umara,huku pia sauti ya Nasra ilizidi kuvurauga akili yangu,.

Na kadri sauti kali ya Nasra ilipokuwa ikipaaa ndani ya kichwa changu ndivyo nguvu zilivyo zidi kuniishia, nikajikuta nakuwa ‘mdebwedo mithili ya teja na

Hatimae nikajikuta napotelea katika bahali ya kiza kizito, huku yule askari wakizidi kunisindikiza kwa maswali lukuki, dakika kadhaa mbele sikujua  kilichoendelea.

 

Je, nini kitaendelea?
Tukutane Ijumaa hapahapa.

 

 

 

 

 

Toa comment