The House of Favourite Newspapers
gunners X

JK Aongoza Maziko ya Mama wa Mwenyekiti CCM Moro

0

 

RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Jakaya  Kikwete,  jana Desemba 24, 2019, ameshiriki mazishi ya mama mzazi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzui (CCM) Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris.

 

Mama Theodora Vasos Kalogeris alifariki dunia Jumapili, Desemba 22, 2019k, katika Hospital ya Chuo cha Kilimo (SUA) Morogoro na kuzikwa jana alasiri makaburi ya Kola Hill Morogoro Mjini.

Mapema viongozi na wanachama walimwaga marehemu na kufanya ibada fupi nyumbani kwake Mji Mpya na baadaye kufuatiwa na ibada ya mazishi Kanisa la Kuu St. Patrick.

Viongozi wengine walioshiriki maziko hayo ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), wabunge kutoka mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Korogwe, Marry Chatanda, wakuu wa wilaya zote za mkoa huo.

Pia, mkuu wajeshi la polisi (IGP) mstaafu, Omari Mahita, wenyeviti wa chama wa wilaya zote wakiongoza kamati za siasa za wilaya zao, na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoa huo.

 

Pa walikuwepo wakuu wa taasisi za umma, ndugu na marafiki.

 

Leave A Reply