The House of Favourite Newspapers

JLo: “Siangalii Umri” – Azungumzia Tetesi Za Yeye Kuwa Kwenye Mahusiano Na Drake – (Video).

Tetesi za Jenifer Lopez (JLo) kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na rapa Drake zimezidi kuvuma na pengine hii interview inaweza kukupa majibu ya maswali yako yote.

Usiku wa Jumanne (Feb.21), Jenifer Lopez alikuwa kwenye kipindi cha Ellen DeGeneres Show ambapo moja ya maswali makubwa aliyoulizwa ni pamoja uvumui wa tetesi za kuwa yupo kwenye mahusiano ya kimapenzi na rapa Drake baada ya picha ya wawili hao kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha wakikumbatiana kama wapenzi.

Hapana, sisi ni marafiki, tulikuwa tu tunaspend time kama marafiki… alisema JLo.

Kuhusiana na uvumi huo, JLo pia alizifuta tetesi za kuwa anapenda kutembea na vijana wadogo, kama vile Drake

Sitembei na wanaume nilyowazidi umri… sio kwamba eti inabidi uwe mdogo kwangu kwa mimi kutembea na wewe. Haihusiani chochote na hilo. Nakutana na watu na ikitokea nimetembea nao, nimetembea nao, na kama nimevutiwa nao, nimevutiwa nao, na kama sijavutiwa nao, ni simple sijavutiwa nao. Ni vile tu mtu alivyo, na sio kuwa yeye ni fulani. Haina uhusiano wowote na umri.

Kwenye interview hiyo na Ellen, JLo alizungumzia pia kuhusu collabo yake na Drake:

Tumefanya wimbo pamoja… Actually, alinitumia wimbo aliopenda anishirikishe, na nikafanya kipande change kwenye huo wimbo. Kwahiyo sijajua ana mpango wa kufanya nini na huo wimbo.

Haijajulikana bado collabo hiyo itatoka lini, ila kwa sasa Drake yupo kwenye ziara yake ya “Boy Meets World” inayoendela kwenye miji mbalimbali Marekani.

Unaweza kuicheki interview ya Jenifer Lopez kwenye kipindi cha Ellen hapa chini.

 

IMEANDIKWA NA: Sandra Brown.

Comments are closed.