The House of Favourite Newspapers

 Joh Makini atoboa siri ya kolabo yake na Davido

0

Joh-makiniStaa wa Hip Hop Bongo anayewakilisha Kundi la Weusi, John Simon ‘Joh Makini’wpid-davido-his-hkn-crew-fly-private-jet-to-kenya-in-style-31

Staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’

STAA wa Hip Hop Bongo anayewakilisha Kundi la Weusi, John Simon ‘Joh Makini’ ametoboa siri ya kolabo yake na staa wa muziki kutoka Nigeria, David Adeleke ‘Davido’ kuwa Davido ndiye alikuwa na shauku ya kufanya naye kolabo na kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii.

Akichonga na Showbiz, Joh Makini alisema, kupitia ukurasa wake wa Instagram, alitumiwa ujumbe mfupi na Davido na kuelezwa kuwa amekuwa shabiki wake mkubwa na angependa wafanye naye kazi.

“Kiukweli nilishangaa sana maana sijawahi kukutana mahali popote na Davido, so lilikuwa jambo la kushtukiza kwangu lakini nikagundua siri ambayo wasanii wengi hawaijui ni kwamba muziki ni lugha inayoweza kuwaunganisha wasanii kutoka kona yoyote ile duniani,” alisema Joh.

Leave A Reply