The House of Favourite Newspapers

Joh Makini, Barnaba Kuongoza Wakali 25 Dar Live

0
Joh Makini.

MKALI wa Muziki wa Hip Hop, Joh Makini pamoja na mkali wa miondoko ya Zouk Rhumba, Barnaba wanatarajiwa kuongoza wakali 25 ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala – Zakhem jijini Dar.

Akizun-gumza na Risasi Vibes, Meneja na Mratibu wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ alisema kuwa usiku huo utatambulika kama Funiko Concert likijumuisha wakali kibao katika Muziki wa Hip Hop, Zouk pamoja na Singeli.

Barnaba.

“Utakuwa ni usiku wa kihistoria tangu Dar Live ianze, mashabiki kwa mara ya kwanza wategemee kuwaona wakali zaidi ya 25 ambao baadhi yao ni Billnas, Barakah The Prince, Moni, Man Fongo, Amber Lulu, Baucha, Pam D, Linex, Jay Moe na Mesen Selekta huku MC akiwa Mr. T Touch na Meneja Maneno,alisema KP. Funiko Concert imedhanimiwa na Global Group kupitia Dar Live.

Stori: Risasi Vibes.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

Leave A Reply