The House of Favourite Newspapers

Omog: Ni Kazi Kuizuia Yanga SC Isikufunge

0
Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog.

KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon, anaiandaa safu yake ya ulinzi kuhakikisha hairuhusu bao katika mchezo wa Jumamosi hii dhidi ya watani zao wa jadi Yanga utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar, huku akisema ni kazi Omog ambaye yupo Zanzibar na kikosi chake cha Simba, anaifanya kazi hiyo kutokana na safu ya ushambuliaji ya Yanga am­bayo kwa sasa inaongozwa na Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa kuonekana kuwa hatari kwa timu pinzani.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Ajibu na Chirwa, mpaka sasa ndani ya kikosi cha Yanga wamefanikiwa ku­funga jumla ya mabao saba kati ya 10 ambayo timu hiyo imeyafunga msimu huu katika mechi saba.

 

Omog ameliambia Cham­pioni Jumatano kuwa: “Nataka katika mchezo wetu dhidi ya Yanga tuweze kutoka uwanjani na ushindi safi am­bao utakuwa na mabao kwa upande wetu lakini si kwa wapin­zani.

 

“Na­jua ni kazi ngumu kumzuia mpinzani wako asifunge kuto­kana na kuwa na wachezaji mahiri, lakini tutajitahidi ku­hakikisha ha­wafungi, lengo ni kupata pointi tatu dhidi yao na si kingine,” alisema Omog.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android Bofya ===> Google Play

iOS Bofya ===>Apple Store

===

Stori: Omary Mdose | Championi Jumatano

Leave A Reply