JOHARI AWA MBOGO RAY KUACHANA NA CHUCHU

Blandina Chagula ‘Johari’

STAA wa sinema za K ibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amegeuka mbogo baada ya kuulizwa ishu ya mpenzi wake wa zamani, Vincent Kigosi ‘Ray’ kudaiwa kumwagana na mzazi mwenzake, Chuchu Hans.  

 

Akichonga na Risasi Jumamosi huku akionekana kuwa na hasira, Johari alisema kwa mwaka huu hataki kabisa kuzungumzia maisha ya Ray na Chuchu kwa sababu yuko bize na mambo yake ya maisha na si kuangalia familia za watu wengine hivyo wanaosema amefurahia wawili hao kumwagana wamuache.

“Yaani sitaki kabisa kuzungumzia masuala ya hao watu, kwa sasa nipo bize na mambo yangu na pia hayanihusu na wala siwezi kusema kwamba sijafurahishwa kwa kuwa sihitaji kabisa kujua na kufuatilia maisha yao,” alisema Johari.

Stori: Neema Adrian, Dar

Toa comment