The House of Favourite Newspapers

Johora Ashusha Presha Yanga Kimataifa

0

MLINDA mlango mpya wa Yanga, Eric Johora amefunguka kuwa matokeo ya mchezo wao uliopita dhidi ya Zanaco yamewapa ari zaidi ya kupambana, kuhakikisha wanafanya vizuri katika michezo yao ijayo hususani mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

 

Yanga Jumapili iliyopita walikuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya
Zanaco ya Zambia katika kilele
cha Wiki ya Mwanachi, mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkapa ambapo Yanga walifungwa mabao 2-1.

 

Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga wanatarajiwa kuwavaa Rivers United ya Nigeria ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Septemba 12, mwaka huu Dar es Salaam, kabla ya mchezo wa marudiano kupigwa Septemba 19, mwaka huu.

 

Johora ambaye ni raia wa Tanzania amejiunga na Yanga akitokea Aigle Noir ya Burundi aliyohudumu msimu uliopita, ambapo ni miongoni mwa nyota 11 wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Johora alisema: “Nimefurahi kukamilisha usajili wangu ndani ya Yanga, kwa muda mfupi ambao nimekuwa hapa nafurahi kuona jitihada za kila mchezaji katika kuhakikisha.

STORI NA JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave A Reply