The House of Favourite Newspapers

Jokate adaiwa kufichwa…

JOKATE_MWEGELO4.jpg
 
 
Hamida hassan, Risasi Jumamosi
 
DAR ES SALAAM: Mwanamitindo, Jokate Mwegelo ametimkia nchini Uturuki ambapo inadaiwa kuwa amepelekwa na mwanaume mmoja wa Kiarabu ambaye walikuwa na mawasiliano naye tangu kitambo.
 
Sosi aliyekaribu na staa huyo, aliliambia Risasi Jumamosi kuwa Jokate ametumiwa nauli na mwanaume huyo ambaye ndiye aliyempokea baada ya kuwasili na sasa wanakula bata pamoja katika viwanja mbalimbali nchini humo.
 
“Si unajua tena madada zetu huwa hawaangalii aliyemuita wanachoangalia wao ni mkwanja na kutembea akiambiwa majuu tu anakwenda bila kujiuliza anapokwenda kama ni heri,” alisema sosi huyo.
 
Mwandishi wetu alipopata habari hii, alimtafuta Jokate kwa njia ya simu ambapo alisema kuwa kweli yupo Uturuki lakini amekwenda kwa ajili ya utalii na kutafuta fursa za kibiashara kwa vijana wa Afrika Mashariki.
 
“Jamani watu wakiona umetoka tu nje ya nchi wanaanza kukuzushia maneno, mwenzao mimi nimekwenda kutalii nimepelekwa na Kampuni ya Skypalm Tours pamoja na Turkish Airlines hayo mambo ya mabwana nawaachia wanaoyaweza mimi huko sipo,” alisema Jokate.
 
Aidha, Jokate alisema kuwa kwa sasa mpenzi wake ni biashara tu na mambo ya maendeleo.

Comments are closed.