The House of Favourite Newspapers

Joseph Msami amtolea povu Mwijaku

0

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Msami amemtolea povu msanii wa filamu Bongo, Mwemba Batoni ‘Mwijaku’ na kusema kuwa aache tabia ya kujifanya ndiye msemaji wa familia za watu.  Akizungumza na Risasi Vibes, Msami alisema kuwa Mwinjaku anajifanya yeye ndiye mfuatiliaji na msemaji wa familia za watu, hivyo anamkanya aache.

“Unajua Mwijaku alikuja THT akiwa mtu wa masoko na alikuwa anajulikana kwa jina la ‘Mwembe’ sasa hili jina la Mwijaku sijui kalitoa wapi na pale THT akajikuta kuwa ana vipaji vingi kuzidi hata aliyewakuta.

Sasa hivi anajifanya ndiye msemaji wa familia za watu Instagram, yaani anajikuta kama nani sijui, mi’ namshangaa sana. Aache tabia hiyo, asitafute umaarufu kwenye familia za watu,” alisema Msami. Mwijaku amekuwa na tabia ya kuzungumzia maisha ya watu hususan katika mambo ya uhusiano na hata akikatazwa huwa hajali, anazidi kuwasema wengine.

Leave A Reply