The House of Favourite Newspapers

JPM Aaanika Madudu Uwanja wa Taifa – Video

RAIS John Magufuli ameitaka Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo  na Wizara ya Mambo ya Nje kupitia vyombo vyake vya ulinzi kuhakikisha tiketi zinazokatwa kwa ajili ya mashabiki kuingia uwanjani, zizingatie idadi halisi ya watu wanaotakiwa kuingia kwentye uwanja huo badala ya kuwarundika na wengine kukosa nafasi za kuingia ilhali wameshawakatia tiketi.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Machi 25, 2019,  Ikulu, Dar es Salaam, alipokutana na wachezaji wa Taifa stars, viongozi wa shirikisho la soka nchini (TFF), iliyokuwa Kamati ya Uhamasishaji iliyofanikisha timu ya soka ya taifa kusonga mbele kwa kuifunga Uganda mabao 3-0 na kupata nafasi ya kushiriki fainali za mashindano ya ubingwa kwa nchi za Afrika (AFCON) yatakayofanyika nchini Misri mwezi Juni.

Vilevile,  fursa hiyo ilitumika kumpongeza bondia Hassan Mwakinyo aliyepata ushindi nchini Kenya kwa kumtoa kwa ‘knockout’ bondia wa Argentina mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katika hafla hiyo ya kuwapongeza rais pia alipata chakula cha mchana na wanamichezo hao.

 

“Ukarabati wa Uwanja wa Taifa haupo vizuri, swali la kujiuliza ni je, hayo makato yanayokatwa yanakwenda wapi?  Je, viongozi wa wizara hawaoni matatizo ya uwanja? Wachezaji wananufaika vipi na timu yao ya taifa?” aliuliza rais  akisema kwamba iwapo uwanja huo unachukua watazamaji wapatao 60,000 lakini wanaingia watu zaidi “je, hizo pesa zipo kwenye akaunti gani?  …Idadi ya watazamaji ilikuwa kubwa, je, hawakujua kuwa kujazana uwanjani ni hatari? Wizara ilijipanga?”

 

Magufuli aliendelea kuuliza iwapo idadi ya tiketi ilikuwa inajulikana na ni kwa vipi nusu ya watuwalikaa nje na tiketi.

 

“Kwa nini nusu ya watu walikaa nje na tiketi?  Kwa nini hakukuwa na kikomo cha tiketi? Je, wangeingia watu laki moja yakatokea maafa wizara ililifahamu hili? Ilichukua hatua gani?” ni miongoni mwa maswali aliyouliza rais. na kuongeza kwamba serikali itatoa Sh. bilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya timu ya taifa.

MSIKIE HAPA JPM

Comments are closed.