The House of Favourite Newspapers

JPM Aivunja Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni

0
Rais Magufuli akiwa na viongozi wengine.

RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amevunja Mamlaka ya Uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA) kuanzia leo Septemba 13, 2017.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, amethibitisha hilo na kusema Rais Magufuli ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa Kigamboni na kuamua kuivunja mamlaka hiyo.

“Usikivu ni sehemu ya utatuzi; hatimaye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli ameridhia uvunjwaji wa Mamlaka ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA),” alisema Mgandilwa.

Wakati huohuo, akizungumza leo katika Ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni, katika hafla hiyo, Waziri wa Ardhi, William Lukuvi, leo amesema Rais Magufuli alikuwa amwemwagiza kuivunja rasmi leo KDA.

Mwezi Juni, mwaka huu Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile. aliiomba serikali kukabidhi majukumu yote yaliyokuwa yakifanywa na KDA kupitia Halmashauri ya Manispaa hiyo ili kuyatekeleza na kuendeleza Mji Mpya wa Kigamboni.

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa Dar

Leave A Reply