The House of Favourite Newspapers

JPM Ammwagia Minoti Mama Ntilie Morogoro – Video

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amempa Tsh. 100,000 mama aliyeibua kero ya kufukuza kwa wafanyabishara ndogondogo za vyakula ‘mama ntilie’ katika stendi ya daladala, Morogoro Mjini.

 

Hayo ameyafanya leo Machi 15, 2018 katika uzinduzi wa kiwanda cha sigara cha Philip Moris mjini Morogoro, alipomruhusu mama aliyejitambulisha kwa jina la Avintushi kueleza kero yake.

 

“Sisi tunafanya biashara ya chakula Stendi ya Hiace Morogoro Mjini, wakubwa hawatuthamini, tunanyang’anywa biashara zetu, tunalipa faini lakini haturudishiwi biashara zetu, tunaadhirika, tunanyanyasika na watoto, tunakosa pa kulala wala chakula, hatuna msaada wowote, tunaomba Mheshimiwa Rais utusaidie,” alisema mama huyo.

 

Baada ya maelezo hayo, Rais Magufli alimtaka Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro kutoa ufafanuzi ambaye naye alieleza kuwa wametenga maeneo maalum kwa ajili ya wafanyabishara hao, alisema kwenye magulio ambako wamewawekea meza rasmi za kufanyia biashara zao.

 

Rais Magufuli alimtaka mkurugenzi huyo kutowabughudhi wafanyabiashara hao waweze kujipatia kipato kwa biashara zao ndogondogo ili kujikwamua kimaisha.

 

“Mimi nimezaliwa na wazazi maskini, nina fafamu hawa wamama huwa wanabeba sinia au ndoo wanapita kwenye mabasi, wasafiri wanaweza kununua chochote mfano karanga, ndizi au maji ambavyo havihitaji meza, hivyo na wao wanajipatia kipato kupitia hapo.

 

“Sasa nakuagiza mkurugenzi, waache wafanye biashara zao, nyinyi mzingatie usafi, tusitumie sababu za ugonjwa wa kipindupindu kuwapa shida watu hawa. JKama tatuizo ni meza, ulitakiwa wewe mkurugenzi uchukue pesa unazokusanya ununue meza hata za vioo ukaweke pale,” alisema Rais na kumruhusu mama huyo anedelee kufanya biashara zake katika stendi hiyo huku.

 

Aidha, Rais Magufuli amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kwebwe na Mkuu wa Wilaya kuhakikisha wanalisimamia suala hilo na kutengeneza mazingira mazuri ya biashara kwa akina mama hao.

 

Baada ya hapo, Rais Magufuli alimpa mama huyo kifuta machozi cha Tsh. 100,000 huku akimwagiza Mkurugenzi wa Mkoa naye atoe Tsh. 50,000. Wengine waliomchangia mama huyo ni Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdul Aziz Aboud, Mama Gertrude Lwakatare, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Wilaya, Waziri wa Viwada, Charles Mwijage, mwekezaji, wageni na wengine waliohudhuria. Hivyo mama huyo kuondoka jukwaani hapo na kitita cha fedha kwa ajili ya kujikimu.

 

Na Edwin Lindege.

VIDEO: SHUHUDIA TUKIO HILO

Comments are closed.