The House of Favourite Newspapers

JPM Ampangia Ubalozi Aliyekuwa Bosi wa TAKUKURU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Richard Faustine Sambaiga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Sambaiga umeanza Machi 23, 2019.

 

Dkt. Sambaiga ni Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha DSM na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rukia Masasi ambaye amemaliza muda wake.

 

Pia, Rais Magufuli leo Machi 28, 2019 atamuapisha Balozi Mteule Valentino Mlowola kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba. Balozi Mteule Mlowola ataapishwa Ikulu Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.

Comments are closed.