The House of Favourite Newspapers

JPM Ampigia Simu Waziri Lukuvi, Atumbua Hadharani! – Video

Rais Dkt John Magufuli, ameendelea na ziara yake ya kutembelea, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria ambapo leo Septemba 05, ametembelea mkoa wa Mara, wilaya ya Bunda na kisikiliza kero kisha kuzungumza na wananchi wa eneo hilo kabla ya kutoa maamuzi ya papo kwa hapo.

 

Rais Magufuli amuagiza Waziri Lukuvi amtumbue Kamishna wa ardhi Kanda ya Ziwa baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu Kwa kushindwa kutekeleza maagizo ya Waziri huyo aliyemtaka kushughulikia mgogoro wa ardhi.

Kamishna huyo aliyejulikana kwa jina moja la Shawio alipewa maagizo ya kutatua mgogoro unaohusu tajiri mmoja kudhulumu ardhi ya bibi mmoja kwa nguvu na kujenga maduka. Bibi huyu aliyekuwa na viwanja viwili, aliuza kimoja ili kupata fedha za matibabu baada ya hapo tajiri mmoja alijenga maduka katika kiwanja kingine kilichobaki.

Waziri Lukuvi alipotembelea eneo hilo alitoa maagizo kwa Kamshina Shawio na Mkuu wa Wilaya kushughulikia suala hilo na kuhakikishia kiwanja hicho kinarudi kwa bibi huyo. Aidha, agizo hilo halikufanyiwa kazi mpaka leo bibi huyo na mjukuu wake walilalamika mbele ya Rais Magufuli

VIDEO: MSIKIE JPM AKIFUNGUKA HAPA

Comments are closed.