JPM Ampongeza TB Joshua Siku Yake ya Kuzaliwa

RAIS John Magufuli amemkumbuka na kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa Mhubiri maarufu Barani Africa, Nabii Temitope Belgun Joshua ‘TB Joshua’ wa Kanisa la Sinagosi la Mataifa Yote lenye makao yake makuu mjini Lagos nchini Nigeria.

 

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Magufuli ameandika;

 

Yaani

“MTUMISHI WA MUNGU, Mchungaji TB JOSHUA Kwa niaba ya familia yangu, ninakupongeza kwa moyo mkunjufu katika kutimiza mwaka wa 55 wa kuzaliwa kwako. Mwenyezi Mungu akupe nguvu kubwa itakayokuwezesha kuwakomboa watu wengi zaidi na kueneza utukufu wake katika mataifa mbalimbali. NAKUTAKIA SIKU NJEMA YA KUZALIWA.”

 

TB Joshua aliwahi kuzuru nchini mwishoni mwaka 2015 baada ya uchaguzi Mkuu na kuzua maswali mengi kufuatia kutua Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar, bila kuwa viatu miguuni huku Rais Mteule (wakati huo) Magufuli akiwa amebakiza siku chache kuapihwa alimpokea kiongozi huyo wa kiroho.

 

JPM AMWAGA TSH. MILIONI 10 CASH UJENZI WA MSIKITI DAR – VIDEO

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment